Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu (katikati) akijadiliana na Makamu wa Rais wa Chuo cha Ufundi Stadi wa Kilimo Henan cha nchini China, Prof. Wu Guozhao (kushoto) na mmoja wa wafanyakazi wa chuo hicho,
Monica (kulia) walipotembelea VETA tarehe 17 Desemba 2019
Makamu wa Rais wa Chuo cha Ufundi Stadi wa Kilimo Henan cha nchini China, Prof. Wu Guozhao akizungumza na Menejimenti ya VETA na wafanyakazi wa Chuo cha VETA
Kihonda Mkoani Morogoro alipotembelea chuoni hapo tarehe 17 Desemba 2019
Timu ya Viongozi na Wataalam kutoka Chuo cha Ufundi Stadi wa Kilimo Henan cha nchini China, Menejimenti ya VETA na wafanyakazi wa Chuo cha VETA Kihonda Mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja kwenye shamba darasa la Chuo cha VETA Kihonda wakati timu hiyo ilipotembelea chuo hicho tarehe 17 Desemba 2019
Dkt. Liu Songtao, Makamu Mkuu wa Shule ya Uhandisi Kilimo ya Chuo cha Ufundi Stadi wa Kilimo Henan cha nchini China akitoa mada kwenye kikao na wafanyakazi wa VETA katika Chuo cha VETA Kihonda mkoani Morogoro, tarehe 17 Desemba 2019
Makamu wa Rais wa Chuo cha Ufundi Stadi wa Kilimo Henan cha nchini China, Prof. Wu Guozhao (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na walimu waliopata ufadhili wa kusoma kozi mbalimbali za kilimo katika chuo chake kuanzia mwaka wa masomo 2020