Mratibu Msaidizi wa Mfumo Pacha wa mafunzo(DATS) kutoka VETA, Challange Fihili akimuelezea namna mfumo pacha wa mafunzo(Dual Apprenticeship Training System-DATS) unaoendeshwa kwa pande kuu mbili zinazohusisha viwanda pamoja na Vyuo vya VETA mmoja wa wananchi waliofika kwenye maonesho ya wiki ya Viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Uhusiano wa VETA Dora Tesha akitolea ufafanuzi kuhusu utengenezwaji wa pochi kwa wananchi waliofika katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere
Mwanafunzi wa VETA Mwaka wa Pili wa Kozi ya Electrical Installation, Omary Japhari akitoa ufafanuzi kuhusu umeme mkubwa unavyofanya kazi katika sehemu mbalimbali kwa wananchi waliofika katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere
Mhitimu wa VETA, Zadock James akitolea ufafanuzi kuhusu ubunifu wa mfumo wa kuchuja maji safi na salama kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye maonesho ya Viwanda yaliyoanza Desemba 05 hadi Desemba 07, 2019.
Mwanafunzi wa VETA wa Mwaka wa Tatu wa Kozi ya Automotive Mechanics, Shafii Kamugisha akiwafafanulia wananchi waliofika kwenye maonesho kuhusu mfumo wa Injini unavyofanya kazi kwenye Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa VETA katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.