Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha
(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
akielezea maandalizi ya mashindano ya riadha kwa wanawake “Ladies First”
yakayoanza Desemba 7 hadi 8,2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha wanariadha toka Tanzania Bara na Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Dk. Hamad Ndee na kulia ni Mwakilishi Mkazi toka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Naofumi Yamamura.
Mwakilishi Mkazi toka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA),
Naofumi Yamamura (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati akielezea maandalizi ya mashindano ya riadha kwa wanawake “Ladies First” yakayoanza Desemba 7 hadi 8,2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha wanariadha toka Tanzania Bara na Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Dk. Hamad Ndee na katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Dk. Hamad Ndee
(kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
akielezea maandalizi ya mashindano ya riadha kwa wanawake “Ladies First”
yakayoanza Desemba 7 hadi 8,2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha wanariadha toka Tanzania Bara na Zanzibar, katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha na kulia ni Mwakilishi Mkazi toka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Naofumi Yamamura.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwakilishi Mkazi toka Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan (JICA), Naofumi Yamamura wakati akielezea maandalizi ya
mashindano ya riadha kwa wanawake “Ladies First” yakayoanza Desemba 7 hadi 8,2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha wanariadha toka Tanzania Bara na Zanzibar.
Picha na BMT
************************************
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japani (JICA) pamoja na Shirikisho la Riadha Tanzania limeandaa mashindano ya riadha kwa wanawake “Ladies First 2019” ambayo yatafanyika tarehe 7 hadi tarehe 8 Disemba, 2019 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mashindano haya yanafanyika kwa mwaka wa tatu, baada ya kufanyika kwa mafanikio makubwa mwaka 2017 na 2018 kwa kuwashirikisha wanariadha wa kike kutoka mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar.
Lengo la mashindano haya ni kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika michezo hususani mchezo wa Riadha, kutoa fursa ya wanariadha wa kike kuonyesha vipaji vyao na kuendeleza vipaji vya wanariadha ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa siku za baadae.
Mashindano ya Mwaka huu yatashirikisha wanariadha wa kike na viongozi zaidi ya 200 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani pamoja na wanariadha kutoka Sudani Kusini ambao wamealikwa pia kushiriki katika mashindano ya mwaka huu. Mashindano haya pia yatashuhudiwa na wanafunzi elfu moja (1,000) kutoka baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari kutoka Manispaa ya Temeke.
Baraza la Michezo la Taifa linaishukuru sana taasisi ya JICA na kampuni za Kijapani zinazofanya kazi nchini Tanzania, kwa kufadhili mashindano haya kwa mwaka wa tatu mfululizo. Baraza linaishukuru pia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutoa Uwanja wa Taifa ambao utatumika katika mashindano hayo pamoja na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambayo imetoa ruhusa kwa wanafunzi wa baadhi ya shule za Manispaa ya Temeke kushiriki katika mashindano hayo.
Aidha, BMT kwa namna ya pekee linampongeza Mjumbe wake, Mwanariadha mstaafu na ambaye pia kwa sasa ni Balozi wa JICA Tanzania Kanali Mstaafu Juma Ikangaa kwani yeye ndie kiunganishi kati ya BMT na JICA ambaye amefanikisha mradi huu wa mbio kwa wanawake nchini Tanzania.
BMT pia linaziomba Kamati za Michezo za Mikoa, zihakikishe zinawezesha ushiriki wa wanariadha wao katika mashindano haya, Kushindwa kushiriki kwa Mikoa kutawanyima fursa wanariadha wao kushindana na wanariadha wengine kutoka mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baraza linaomba wananchi wote wa Wilaya ya Temeke na maeneeo yote ya Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya mashindano kuwashangilia na kuwapa hamasa wanariadha wetu wa kike, kwani mashindano hayana kiingilio chochote ni bure kabisa