Home Michezo Tanzania yashika nafasi ya Pili Mashindano ya Mpira wa Meza kwa Wanawake...

Tanzania yashika nafasi ya Pili Mashindano ya Mpira wa Meza kwa Wanawake Afrika Mashariki

0

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza (TTTA), Issa Mtalaso akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kukabidhi kombe la mshindi wa pili wa mashindano ya mpira wa meza kwa wanawake Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda, kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha (kulia) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa pili wa mashindano ya mpira wa meza kwa wanawake Afrika
Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda, Neema Mwaisyula (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha.

Mshindi wa pili wa mashindano ya mpira wa meza kwa wanawake Afrika
Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda, Neema Mwaisyula (katikati) akimkabidhi
kombe Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha
(kulia) katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza (TTTA), Issa Mtalaso.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha
(kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea kombe toka kwa Mshindi wa pili wa mashindano ya mpira wa meza kwa wanawake Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda, Neema Mwaisyula.

Mshindi wa pili wa mashindano ya mpira wa meza kwa wanawake Afrika
Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda, Neema Mwaisyula (katikati) akizungumza na waandi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi kombe kwa kombe Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha (kulia) na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza (TTTA), Issa Mtalaso.

Picha na BMT