Wajumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira (UNEP) Bi Victoria Panadero na Bi Kelly West wakichangia wakati walipokutana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Joseph Malongo walipomtembelea Ofisini kwake kujadili kuhusu Mradi wa Kurejesha uoto wa asili katika maeneo ya ardhi yaliyoharibika.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Joseph Malongo pamoja na Watumishi wa Ofisi yake akiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira (UNEP) wakati walipomtembelea Ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Lengo la kikao hiko ni kujadiliana mambo yahusuyo mzingira ikiwemo mradi wa kurejesha uoto wa asili katika maeneo yaliyoharibika.