Wanafunzi wa Skuli ya Kilimahewa ‘B’ Hafidhuu Saidi na Dhulkifli Omar Kombo wakielezea mafanikio waliyoyapata katika ziara ya kutembelea makumbusho huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge Mjini Zanzibar.
Picha ya Pamoja ya Wanafunzi na Walimu wa Skuli ya Kilimahewa ‘B’ huko Mnara wa Kumbukumbu Kisonge Mjini Zanzibar.
Msaidizi wa Mwalimu Mkuu Skuli ya Kilimahewa ‘B’ Mwanamke Ahmada Khamis akielezea kuhusu ziara ya Wanafunzi wa Skuli ya Kilimahewa ‘B’ kutembelea sehemu ya makumbusho huko Mnara wa Kumbukumbu Kisonge Mjini Zanzibar.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
*******************************
Wazazi na walezi wametakiwa kwenda Skuli mara kwa mara ili waweze kubaini matatizo yanayo wakabili watoto wao na kuweza kuyapatia ufumbuzi wa haraka .
Wito huo umetolewa na Msaidizi wa Mwalimu Mkuu wa skuli ya kilimahewa B Mwamke Ahmada khamis wakati alipokuwa katika ziara ya kimasomo huko katika Makumbusho ya kumbukumbu ya mapinduzi kisonge wilaya ya mjini unguja
Amesema wanafunzi wanakabiliwa na matatizo mbali mbali wakati wanapo kuwa skuli lakini yanashindwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kutoa ushirikiano pale ambapo wanahitajika .
Aidha amesema kuna baadhi ya wanafunzi wanakuwa na ufahamu mdogo katika masomo yao hivyo wanahitaji uangalizi wa hali ya juu kutoka kwa wazazi na walimu kuwa pamoja .
Mwalimu Mwamke amefahamisha ni vyema kwa wazazi kuto kuona ugumu kwenda skuli mara kwa mara kwani kuna mpa fursa kutambua maendeleo ya mtoto wake na kumfanya wanafunzi kupata matokeo mazuri katika mitihani yake .
Sambamba na hayo amewataka kutowaruhusu kujitia manukato wakati wanapo kwenda skuli ili kuwanusuru na matatizo ambayo yanaweza kuwatokea ikiwemo vitendo vya udhalilishaji
Wakati huo huo amewataka wazazi kutotilia uzito suala la kuwapa pesa watoto wakati wanapo hitaji kwenda katika ziara za kimasomo ili waweze kupata fursa za kujifunza kivitendo na kutambua historia ya nchi yao .
“ Wazazi na walezi tujitahidi kuwapa watoto wetu pesa za kwenda kwenye ziara za kimasomo kwani huko wanapata fursa za kujifunza kwa vitendo na kutambua mambo mengi yaliyo kuwemo ndani ya nchi yao “ Alisema Msaidizi huyo .
Kwa upande wake Mwalimu wa somo la Historia Amina Salum Suleiman amesema ziara za kimasomo zina umuhimu mkubwa kwani zina wapa fursa watoto kutembea maeneo mbali mbali ya kihistoria na kuweza kuelewa kwa ufasaha .
Hata hivyo ameiomba Wizara ya Elimu kuwapatia walinzi katika skuli yao watakao weza kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao .
Akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wenziwe Hafidhu Saidi amesema ziara hiyo ni nzuri kwani imewafanya waweze kutambua mambo mbali mbali na kuwataka Walimu kizifanya ziara hizo mara kwa mara kwani zina wasaidia kuweza kujibu vizuri mitihani yao.