Mh Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu pamoja na Mkuu Wa Wilaya ya
Kilosa Mh Adamu Mgoyi na baadhi ya wananchi wa kijiji cha mabana kata ya
mbigiri wakizungumza na wananchi kabla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa
mradi wa umeme wa rea katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza wilayani
kilosa mkoani morogoro .
Mh Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(kulia) pamoja na Mkuu wa
Wilaya Ya Kilosa Mh Adamu Mgoyi (mwenye shati ya draft )na baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme
wa rea katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza katika kijiji cha mabana kata ya mbigiri wilaya ya kilosa mkoani morogoro hapo jana .
Mkuu Wa Wilaya Ya Kilosa Mh Adam Mgoi (Aliesimama) Akizungumza Na
Wananchi Wa Kata Ya Mvuha Ndani Ya Wilaya Hiyo Baada Ya Ugeni Wa Naibu
Waziri wa Nishati Mh Subira Mgalu Kutembelea Wilaya Hiyo.
Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Makwambe Kata Ya Mvumi Wilayani
Kilosa Wakimskiliza Naibu Waziri Wa Nishati Bi Subira Mgalu Alipotembelea Kijiji
Hicho.
*********************************
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.
Wakandarasi Wa Mradi Wa Rea Katika Awamu Ya Tatu Mzunguko Wa Kwanza
Wametakiwa Kutekeleza Majukumu Yao Kikamilifu Ili Kufanikisha Adhma Ya
Serikali Ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo Katika Maeneo Yao Ikiwa
Uunganishwaji Wa Umeme Huo Katika Vijiji Utaleta Manufaa Makubwa
Ikiwemo Uuanzishwaji Wa Viwanda Vidogo Vidogo Kuelekea Uchumi Wa Kati.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Naibu Waziri Wa Nishati Bi Subira Mgalu
Alipotembelea Katika Kijiji Cha Mabana Kata Ya Mbigiri Wilayani Kilosa
Mkoani Morogoro Kwa Ajili Ya Uzinduzi wa Uwashaji Wa Umeme, Na kuongea
na wananchi wa kijiji Makwambe Kata Ya Mvumi Wanaotarajiwa Kupatiwa
Umeme Kupitia Mradi Huo.
Mh.Mgalu Amesema Kumekuwa Na Malamiko Mengi Kutoka Kwa Wananchi
Hasa Kuhusu Michoro Inayoidhinishwa Na Bodi Katika Uwekaji Wa Nguzo Za
Umeme Hivyo Limekwisha Tatuliwa Tatizo Hilo Na Kama Wizara Wametoa
Maelekezo Ya Namna Ya Michoro Hiyo Kama Ilivyoidhinishwa Na Bodi Ya
Wakala Wa Vijijini Rea.
Kwa Upande Wake Kaimu Meneja Tanesco Bw.Martin Schilima Na Mkuu Wa
Wilaya Ya Kilosa Mh Adam Mgoi Wameishukuru Serikali Kupitia Naibu Waziri
Mh Subira Mgalu Kwa Hatua Na Jitihada Zinazofanyika Katika Kuwafikia
Wananchi Kwa Kuwaunganishia Umeme Na Kuahidi Kushirikiano Nao Pamoja
Na Wananchi Kwa Kila Hatua Ili Kuwafikia Kwa Wakati.
Nao Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Mabana Kata Ya Mbigiri Wametoa
Shukrani Zao Kwa Kuwashiwa Umeme Katika Kijiji Hicho Na Kuahidi Kufanya
Makubwa Katika Kuwaletea Maendeleo Hasa Uanzishwaji Wa Viwanda Vidogo
Vidogo Kama Kusindika Nyanya.
Mradi Huu Upo Katika Awamu Ya Tatu Mzunguko Wa Kwanza Ambapo Kuna
Vijiji Mia Moja Na Sitini Na Tano Katika Mkoa Wa Morogoro Ambapo Katika
Wilaya Ya Kilosa Kuna Vijiji 24 Na Mpaka Sasa Vijiji Kumi Vimeshawashwa
Umeme Na Vijiji Vilivyosalia Kumi Na 4 Vinakwenda Kuwashwa Umeme Kabla
Ya Mwezi Desember Mwaka Huu.