Home Mchanganyiko MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE ATOA KOMPYUTA KWA WANAHABARI SINGIDA

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE ATOA KOMPYUTA KWA WANAHABARI SINGIDA

0
Katibu wa Mbunge wa Viti Maalumu ( CCM) Mkoa wa Singida, Mariam Ntembo (kulia), akimkabidhi Kompyuta Mwenyekiti wa  Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (Singida Press Club), Seif Takaza aliyoitoa mbunge  huyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari hao katika shughuli zao za  kila siku. Katikati ni Katibu wa Chama hicho, Revocatus Phinius.
*******************************
 
Na Dotto Mwaibale, Singida.
 
MBUNGE wa Viti Maalumu ( CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ametoa kompyuta moja kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (Singida Press Club)
 
Akikabidhi kompyuta hiyo kwa niaba ya mbunge huyo katika mkutano wa kawaida wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki, katibu wa mbunge huyo, Mariam Ntembo alisema kompyuta hiyo imetolewa na Mattembe ili kuwasaidia katika shughuli za kila siku za waandishi wa habari wa mkoa wa Singida.
 
” Mbunge Mattembe amenituma nije kuwakabidhi kompyuta hii kwani anatambua mchango wenu wa kuhabarisha umma kupitia kalamu zenu juu ya maendeleo ya mkoa wetu wa Singida na Taifa kwa ujumla” alisema Ntembo.
 
Ntembo alisema Mbunge Mattembe yupo pamoja na waandishi hao na kuwa anawapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwa ataendelea kukisaidia chama chao kadri atakapopata nafasi ya kufanya hivyo ambapo pia alichangia shilingi laki mbili kwa ajili ya kuwezesha mkutano huo.
 
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Seif Takaza akipokea msaada huo alimshukuru mbunge huyo kwa kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari wa mkoa huo na kumuomba wakati mwingine asisite kuwapa msaada.