Home Siasa CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI CHASEMA TUTAPATA USHINDI WA “KISULISULI” KATIKA UCHAGUZI WA...

CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI CHASEMA TUTAPATA USHINDI WA “KISULISULI” KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

0

Mwenyekiti wa Chama hicho Mohammed Abdula akizungumza na waandishi wa habri katika makao makuu ya chama hicho Mabibo jijini Dar es salaam leo.

Mwenyekiti wa Chama hicho Mohammed Abdula na waandishi wa habri katika makao makuu ya chama hicho Mabibo jijini Dar es salaam leo kulia ni Salim Elias Katibu Mwenezi Chama cha Demokrasia Makini na kushoto ni Coster Kibonde Naibu Katibu Mkuu Bara chama cha Demokrasia Makini.

…………………………………………………….

Chama cha  Demokrasia Makini kimesema ili kujihakikishia ushindi wa “Kisulisuli” kwa wagombea wake wote, viongozi wote wa ngazi ya juu ya chama hicho wamegawana  kwa kila mmoja kwenda katika mkoa wake na kufanya kampeni kwa kadri wanavyoweza kwa kushirikiana na wagombea pamoja na wanachama waliopo katika mikoa hiyo ili kupata ushindi wa Kisulisuli katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji  na vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Chama hicho Mohammed Abdula wakati akizungumza na waandishi wa hanbari kuhusu maandalaizi ya kampeni hizo kuelekea  uchaguzi unaotarajiwa kufanyika ujao katika ofisi za chama hicho zilizopo Mabibo jijini Dar es salaam.

Mohammed Abdula  ameitaja  mikoa ambayo chama hicho kjimesimamisha wagombea kuwa ni pamoja na Morogoro,Mara, Tabora, Kigoma pamoja na Dar es Salaam na kusisitiza kuwa tayari mipango kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni hizo imeshakamilika kwa asilimia mia moja.

“Tutazindua  rasmi kampeni zetu za uchaguzi wa Serikali za mitaa Kilosa katika mkoa wa Morogoro na tutaibuka na ushindi wa’Kisulisuli’ katika maeneo yote ambayo tumesimamisha wagombea wetu” . Amesema Mohamed Abdula.

Abdula amesema kumejitokeza kwa baadhi ya vyama kususia uchaguzi huo, kwa upande wa chama hicho hakina mpango huo zaidi kimeamua kuelekeza nguvu zake kuwapigia kampeni kabambe wagombea wake zaidi ya 80 waliopo nchi nzima ili waweze kibuka na ushindi.

“Kutoshiriki uchaguzi ni kujinyima haki ya kidemokrasia, sisi kama chama makini hatuoni sababu yoyote ya kususia  uchaguzi huu zaidi tumeamua kwenda kushiriki kikamilifu na mipango yetu ni kuondoka na ushindi katika maeneo yote ambayo wagombea wetu watasimama” alisema Abdula.