Home Biashara TBS IMEANZISHA ZOEZI LA KUWAFIKIA WENYE VIWANDA PAMOJA NA WAZALISHAJI WA BIDHAA...

TBS IMEANZISHA ZOEZI LA KUWAFIKIA WENYE VIWANDA PAMOJA NA WAZALISHAJI WA BIDHAA NCHINI NA KUWAPATIA ELIMU

0

Mkaguzi wa Shirika la Viwango Tanzania Bw.Vincent Meleo akitoa elimu kwa wamiliki wa maduka ya vipodozi eneo la soko kuu mkoani Singida namna ya kujisajili katika mfumo ili kuweza kupata kibali kwa ajili ya duka la vipodozi.

Mkaguzi wa Shirika la Viwango Bw Dominisiano Rutahala akitoa elimu kuhusu umuhimu wa bidhaa zinazozalishwa kupata alama ya ubora kwa mwenye kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti kilichopo Kiomboi mkoani Singida.

*********************************

Shirika la Viwango Tanzania TBS ipo kwenye zoezi la kuwafikia wenye viwanda na wazalishaji kote nchini ambao bidhaa zao hazijathibitishwa kuwapatia elimu,kuwasikiliza na kuwasaidia kufikia Viwango.

Hata hivyo Zoezi hilo limeanza kufanyika katika mkoa wa Singida katika Manispaa ya Mkoa huo, Kiomboi na linaendelea katika maeneo ya Manyoni, Mkalama, Shelui,Ikungi na Itigi.

Pamoja na hayo TBS sasa inatumia mfumo ambao unawawezesha wafanyabiashara popote walipo kuweza kupata huduma kirahisi ikiwemo kupata vibali mbalimbali hivyo kuongeza ufanisi na urahisi wa utoaji huduma