Home Mchanganyiko WAZIRI WA MADINI ASHIRIKI KUJADILI CHANGAMOTO ZA BARABARA MKOANI GEITA

WAZIRI WA MADINI ASHIRIKI KUJADILI CHANGAMOTO ZA BARABARA MKOANI GEITA

0

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Grbriel Akiwasilisha Mada katika kakao cha Bodi ya Barabara Mkoani Geita.

Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko akiandika faarifa katika kikako cha Bodi ya. Barabara kilichofanyika Mkoani Geita.

…………………..

Na Tito Mselem Geita,

Waziri wa Madini Doto Biteko ameshiriki katika Kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Oktoba 15,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ili kujadili changamoto za barabara mkoani hamo.  

Kikao hicho kiliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapindizi wakiwemo Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Geita akiwemo Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Doto Biteko, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma, Mbunge wa Mbogwe Augustino Masele, Mbunge wa Busanda Lolesia Bukwimba, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema Pendo Peneza.

Vingozi wengine walioshiriki ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mjini Josephat Maganga, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Mkumba, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe. Martha Mkupasi, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Geita Alhaji Said Kalidushi pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali.

Aidha Waziri Biteko amewapongeza viongozi wa TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri wayoifanya katika Mkoa wa Geita kwa kuhakikisha kuwa barabara zinatengenezwa kwa kiwango kizuri na kumalizika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Biteko amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri katika kuhakisha barabara za Mkoa wa Geita zinakamilika kwa muda uliopangwa na zinakuwa kwenye viwango vinavyotakiwa.

Imeelezwa kuwa Mji wa Geita ni kati ya miji inayokua kwa kasi sana sambamba na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi, hivyo kuwepo na msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu barabarani. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema katika awamu hii ya tano Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitupa ahadi ya ujenza wa barabara na ametekeleza ujenzi wa barabara ya Ushirombo mpaka Lusahunga kilometa 110 kwa gharama ya shilingi bilioni 114.557, Uwanja wa Ndege wa Chato kilometa 3.5 kwa gharama ya Shilingi Billioni 39.15.  

Aidha, Mhandisi Gabriel amesema kwamba, kazi ambazo zimekamilika ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Runzewe  mpaka Bwanga kilometa 45 kwa gharama ya shilingi bilioni 43.357 na barabara ya Bwanga mpaka Biharamuro kilometa 65.0 miradi yote hii inatekelezwa kwa fedha za serikali.

Katika hatua nyingine Mhandisi Gabriel ameeleza kwamba katika Mkoa wa Geita TANROADS inasimamia miradi ya usanifu wa kina katika barabara za Geita mpaka Kahama yenye kilometa 139.557 kwa gharama ya shilingi bilioni 440 inatelekezwa na mkandarasi ENV Engeneering, kazi imekamilika. 

“TANROADS inasimamia pia usanifu  katika barabara ya Nyamirembe mpaka Katoke yenye urefu wa kilometa 50 kwa gharama ya shilingi bilioni 861.046 na Mhandisi Consult ambapo kazi hiyo imekamilika,” Gabriel amesema Mhandisi Gabriel.

Katika hatua nyingine Mhandisi Gabriel ametoa rai kwa wananchi kutunza miundombinu ya barabara kwa kutopitisha mifugo na kunyofoa alama za barabarani pamoja na kutovamia hifadhi za barabara.

Katika bajaeti ya mwaka 2018/2019 TARURA Mkoa wa Geita  unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi 6,844,393,140.37 kutoka mfuko wa barabara (Road fund) kwa ajili ya matengenezo ya barabara na shilingi 1,612,500,000.00 kwa ajili ya kazi za maendeleo, fedha hizo ni kutoka OR-TAMISEMI. 

Hadi kufikia Tarehe 03/01/2019 jumla ya shilingi 2,249,253, 616.84 sawa na asilimia 32.86 zimepokelewa kwa ajili matengenezo ya barabara na jumla  ya shilingi 612,654,524.43 sawa na asilimia 37.99 zimepokelewa kwa ajili ya miradi maendeleo ya barabara za mkoani Geita.