Home Siasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yakutana na Wadau wa Uchaguzi Dodoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yakutana na Wadau wa Uchaguzi Dodoma

0

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano Kati ya Tume na wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma, kuelekea kuanza maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Dodoma.Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera, akizungumza wakati wa mkutano Kati ya Tume ya uchaguzi na Wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma, kuelekea kuanza maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage, katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Dodoma, Mara baada ya kufungua mkutano Kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage, katikati akiwa na wahariri wa vyombo vya habari Mkoa wa Dodoma, baada ya kufungua mkutano Kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa uchaguzi Jijini Dodoma.

…………….

Na.Boniphace Richard

Tume ya taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema imekamilisha maandalizi yote ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Dodoma, huku wakibainisha kuwa ili kupata mafanikio katika zoezi hilo linahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau.

Na ili kuhakikisha elimu ya mpiga kura inawafikia wananchi kikamilifu, wametoa vibali kwa asasi zisizokuwa za kiserikali katika kueneza elimu hiyo katika jamii.

Haya yamebainishwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (rufaa) Semistocles Kaijage, wakati wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi katika jiji la Dodoma wakiwamo wahariri wa vyombo vya habari asasi za kiraia, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Amesema tume tayari imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Dodoma maandalizi yake yamekamilika zoezi hilo linategemea ushirikiano wa wadau mbalimbali .

“Lengo la kukutana nanyi leo ni kuwafahamisha kuwa tume imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoa wa Dodoma na tunaamini mafanikio ya zoezi hilo linategemea ushirikiano wa wadau” amesema Jaji Kaijage.

Aidha amebainisha kuwa zipo asasi za kiraia ambazo zimepewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura kwa madhumuni hayo, hivyo wananchi watakapoona asasi hizo watumie nafasi hizo kujifunza  kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema kwa upande wa Mkoa wa Dodoma zoezi la uhakiki liliongeza vituo vya uandikishaji wa daftari l kudumu la wapiga kura kutoka vituo 2,606 vilivyokuwemo mwaka 2015, hadi kufika 2,686, hivyo kuwa na ongezeko la vituo 80.

Zoezi hilo lilizinduliwa July 18, 2019 Mkoani Kilimanjaro, na baada ya uzinduzi huo zoezi hilo liliendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali, pia baada ya mwaka 2015, tume imekamilisha zoezi kwa awamu ya kwanza katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara, Simiyu,Mara,Mwanza,Geita,Shinyanga,Kagera na Kigoma.

Huku akibainisha kuwa ya Tabora,Katavi,Rukwa na Dodoma zoezi hilo likiwa bado kinaendelea, uboreshaji kwa mwaka huu utafanyika kwa kutumia Technolojia ya kielectronic ya Biometriki(BVR) mfumo huo itachukua taarifa za mtu za kibaiolojia na kuzihifandhi katika kanzi data.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt Wilson Mahera, amesema tume ya taifa ya Uchaguzi imepewa jukumu la kikatiba la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge kwa Jamhuri ya Muungano, na Madiwani kwa Tanzania bara.

Na kwa kila Kijiji/Mtaa kutakuwa na angalau na kituo kimoja cha kuandikisha wapiga kura, na vituo vya kuandikisha wapiga kura vimepangwa katika majengo ya Umma na maeneo ya wazi.