Home Mchanganyiko DC IKUNGI ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI...

DC IKUNGI ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA SINGIDA

0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiangalia papai
alipokuwa akitembelea mabanda 
ya maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo
kitaifa yanafanyika Uwanja
wa Bombadia mkoani Singida.
Mratibu wa maonesho hayo, Sadoti Makwaruzi (katikati) akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Wilaya 
ya Ikungi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya maonesho hayo
na utoaji elimu wa matumizi
ya vyakula vyenye virutubisho.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo,
Revocatus Kasimba (kushoto) 
akitoa taarifa kuhusu hali ya chakula nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo  akizungumza na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) alipotembelea banda lao. Kutoka kushoto
Mtafiti Msaidizi wa Zao la Maharage Tari Selian Arusha, Mtafiti wa Kilimo kutoka Tari Makao Makuu Dodoma, Mshaghuley Ishika na Demetria Mugunda, Mtafiti wa Zao la Maharage
kutoka Tari Selian Arusha, Edith Kadege.
 Afisa Kilimo Wizara Kilimo Idara ya Afya ya Mimea ( PITS)
Twaha Balali 
(kushoto).akimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi matumizi ya
dawa za kuua 
waharibifu wa mazao. 
 Mushema Ayubu kutoka Wizara ya Kilimo Dodoma akimuelekeza
kuhusu matumizi ya mbegu Mkuu 
wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alipotembelea banda
hilo.

Na Dotto Mwaibale, Singida
TAFITI zinazofanywa na wataalamu wa kilimo wametakiwa kuzipeleka kwa wananchi badala ya kubaki nazo ofisini ili zikawasaidie wananchi. 
 
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula kitaifa Mkoani Singida.
 
Alisema wataalamu hao wanapaswa kutoa semina mbalimbali kwa maafisa ugani huko Wilayani ili na wao wakawasaidie wananchi kupata utaalamu mbalimbali wa masuala ya kilimo. 
 
Mpogolo ameyapongeza mashirika ya Save the Children Tanzania,WFP, na FAO kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika masuala ya kilimo, huku akiweka bayana hali ya upatikanaji wa chakula katika wilaya yake kuwa  inachakula cha kutosha,kinachopaswa ni wananchi wake kupatiwa elimu ya lishe bora. 
 
Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo,  Revocatus Kassimba alisema maonesho hayo yanatoa hamasa ya ulaji wa vyakula bora na kuwapa elimu wananchi kuhusu vyakula vyenye virutubisho.