Home Michezo SIMBA YAICHAPA 1-0 BANDARI YA KENYA MECHI YA KIRAFIKI

SIMBA YAICHAPA 1-0 BANDARI YA KENYA MECHI YA KIRAFIKI

0
Na.Alex Sonna,Dar es Salaam
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara timu ya Simba imeendeleza wimbi la ushindi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kuichapa bao 1-0 Bandari FC kutoka nchini Kenya mchezo wa kirafiki.
Shujaa wa Simba ni Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 76 akimalizia pasi ya mshambukiaji chipukizi  Rashid Juma.
 
Simba wanaendelea kupasha misuli kwa kucheza mechi za kirafiki kutokana na Ligi kuu kusimama kupisha mechi za kimataifa ambapo Tanzania ipo ugenini kucheza na Rwanda huku ikitarajia kurudiana na Sudan kuwania kufuzu michuano ya Chan mwakani.
Timu ya Bandari inayofundishwa na Mchezaji wa Zamani wa Yanga,Ben Mwalala akikiandaa kikosi chake kucheza mchezo wake wa kwanza kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Horoya ya Guine anayocheza Herieth Makambo mchezaji wa zamani wa Yanga.
Baada ya mchezo wa Leo, kikosi cha Simba SC chini ya kocha wake Mbelgiji, Patrick Aussems kitaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa ajili ya michezo miwili zaidi ya kirafiki, dhidi ya Mashujaa FC Jumatatu na Aigle Noir FC ya Burundi Jumatano Uwanja wa Lake Tanganyika.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Benno Kakolanya, Haruna Shamte, Joseph Peter/Yusuph Mlipili dk46, Tairone Santos, Paschal Wawa, Gerson Fraga ‘Viera’, Deo Kanda, Sharif Shiboub, Wilker Da Silva/Said Ndemla dk57, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata.
Bandari FC; Michael Wantika, Atariza Amai, Fred Wilata, Brian Otieno, Felly Mlumba, Collins Agade, Patrick Mugendi/Cliff Kasuti dk46, Willy Lugogo, Wycliffe Ochomo, William Wadri na Darius Msagita/Simban Kenga dk46.