Home Siasa ALAT YAONYA RUSHWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

ALAT YAONYA RUSHWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

0

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania, ALAT, Bw. Elirehema Kaaya,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania, ALAT, Bw. Elirehema Kaaya,akijiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura uchaguzi wa Serikali za mitaa katika Mtaa wa Mlimwa Area D jijini Dodoma

……………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Wakati Zoezi la uandikishaji wa daftari la orodha ya  wapiga kura likiendelea  nchini Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania, ALAT, imewaonya wananchi kutokujihusisha na  vitendo vya rushwa, ubaguzi na unyanyapaa katika uchaguzi serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

Pia wananchi wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika orodha ya  daftari la wapiga kura, kwani uchaguzi huo ni mhimu Sana kwao kwani ndio viongozi watakao ishi nao muda wote.

Onyo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania, ALAT, Bw. Elirehema Kaaya, wakati akizingumza na wanahabari, amesema hawatarajii kuona vitendo vya rushwa na ubaguzi na kutoa onyo kwa atakayejihusisha na vitendo hivyo.

“Kuelekea uchaguzi huu tunaonya watu wajiepushe na vitendo vya rushwa, ubaguzi wa kidini,kijinsia, rangi, au kabila na unyanyapaa wowote ule kwa mtu yeyote” amesema Kaaya.

Amesema uchaguzi huo ni wa mhimu sana kwa sababu viongozi wanaochaguliwa ndio wasimamizi wa ulinzi na usalama na ndio wanaoishi nao kila siku hivyo amewataka kutokukosea kuchagua.

Aidha amebainisha kuwa mtu yeyote anayetarajia kugombea nafasi yoyote ni lazima ajiandikisha lasivyo atakuwa amejikosesha kula moja katika uchaguzi huo kwani yeye hatakuwa na nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi huo amesema watu  mwenye sifa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.

” Zoezi hili limeanza tangu tarehe 8 hadi 14 mwezi huu hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha, Kisha kugombea nafasi hizo na Kama unataka kugombea nafasi yoyote hakikisha unajiandikisha lasivyo utakuwa umekosa sifa ya kupata kura yako” amesema.

Pia ameweka wazi kuwa kadi ya mpiga kura haitatumia katika kupiga kura, amesema ni lazima ujiandikishe kwenye orodha ya daftari ya wapiga kura ndipo utakuwa na nafasi ya kupiga kura.

Amewataka maeneo yote ambayo wanatoa matangazo kwa magari wahakikishe Yale yanayotangazwa yawe yameandikwa tena kwa maandishi yanayosomeka vizuri ili kuepusha upotoshaji kwa wananchi kwenye matangazo hayo.