Home Michezo MWAKYEMBE AMPONGEZA MKUU WA MAJESHI KULETA MAPINDUZI KWENYE GOFU

MWAKYEMBE AMPONGEZA MKUU WA MAJESHI KULETA MAPINDUZI KWENYE GOFU

0

**********************************

Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo  Dk Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania  kwa kuendeleza Mchezo  wa Golf nchini ambao umekuwa ukileta heshima kubwa kwa ushindi  Ndani na Nje ya nchi hasa kwa Timu ya Wanawake.

Waziri Mwakyembe alisema hayo Mwisho wa Wiki Akifunga mashindano ya Wazi ya wanawake Tanazania Ladies Open   yaliyoshirikisha Wachezaji zaidi ya 50 kutoka Kenya Uganda na Wenyeji Tanzania  katika Uwanja wa TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro

Waziri Mwakyembe alisema analishukuru JWTZ  anashukuru Mkuu wa majeshi Jenerali  Venance Mabeyo na Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu kwani amekua akishuhudia  mapinduzi makubwa ya Mchezo huo kwa Timu ya Lugalo ikiibuka na Ushindi mkubwa katika mashindano Mengi sambamba na mashindano yanayoshirikisha Timu ya Taifa ya Gofu Lugalo wakiwemo. .

Aliongeza kuwa sasa wanaangalia nini cha kufanya kwa kundi la Wanawake wakiwemo wachezaji wanawake wa Gofu kutokana na mafanikio ya Timu hizo zinzposhiriki katika mashindano ya Kimataifa ukilinganisha na Wanaume.

“ Jeshi linafanya kazi Kubwa na niseme tu Timu za Wanawake ndio timu Pekee zilizotuletea heshima na Vikombe kwa Mwaka huu ikiwemo Timu ya Taifa ya Golf na Timu ya Golf ya Lugalo lakini pia katika Soka ni  Wanawake na Katika  Mpira wa magongo hivyo lazima kuwapongeza na kuwaunga mkono” Alisema Waziri Mwakyembe.

Katika mashindano hayo ya Wanawake Klabu ya Gofu ya JWTZ  ya imenyakua Vikombe nane kati ya 15 katika Mashindano wakiongozwa na  Angel Eaton aliyeshika nafasi ya Tatu kwa  mikwaju  gross  235  na Hawa Wanyenche aliyeshika nafasi ya Nne  kwa Gross ya 236 baada ya Mchuano Mkali na  Peace  Kabasweka  aliyepata Mikwaju Gross  226 kuibuka na Ushindi akifuatiwa na  Irene Nakalembe kwa Mikwaju 232 wote kutoka Uganda

Kwa upande wa kundi la Bronze ambalo kwa kupiga mikwaju  washindi ni Private  Hadija Selemani  aliyefatiwa na Private Amanda Mlula  na  watatu ni  Private Zumla Hamisi huku uande wa Mikwaju ya Jumla  kwa kundi la Silver  na Bronze  Salma Juma wa Lugalo aliibuka na Ushindi wa kwanza akifuatiwa na Happy Castro naye wa Lugalo.

Kwa upande wa watoto Mchezaji wa Lugalo  Christina  Charles aliibuka mshindi huku nafasi ya Pili ikichukuliwa na Aaraji Somji wa Klabu ya Arusha Gymkhana.

Vikombe vingine ni  Washindi wa Kila Siku ambapo Siku ya Kwanza  Merci Nyanchama wa  Kenya aliibuka na Ushindi wakati siku ya Pili Neema Ulomi wa Arusha alishinda na Siku ya Tatu  Nancy Wairimi kutoka Kenya aliongoza.

Kwa Upande wake rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake TLGU Sophia Vigo aliomba wadhamini kuuunga mkono jitihada za wachezaji wa Gofu kwani kwa miaka Zaidi ya Sita hakukuwa na Mashindano kama haya.

Naye Mwenyekiti wa  Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu aliwataka Wachezaji Wanawake kuendelea kupambana na kuwakilisha nchi vyema kwani mambo mazuri huja baadaya ya kazi nzuri na uwepo wa Waziri mwenye dhamana katika Mashindano yao ni Ishara Wametambuliwa juhudi zao.

MW ISHO.