Home Siasa MBUNGE GIGA AKABIDHI FOTOKOPI MASHINE NA PRINTA MKOANI ARUSHA.

MBUNGE GIGA AKABIDHI FOTOKOPI MASHINE NA PRINTA MKOANI ARUSHA.

0

…………………………………………..

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Umoja wa Wazazi Tanzania wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi Anayetokea Zanzibar,Najma Murtaza Giga,Amekabidhi Kompyuta,Fotokopi Mashine na Printa kwa Ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Wazazi ya Mkoa wa Arusha,Mwishoni mwa Wiki, Mbele ya Katibu Mkuu wa Jumuiya Hiyo Taifa,Erasto Sima.

Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Vifaa Hivyo, Mbunge Giga, Alisema Kuwa Ili CCM Iweze Kuimarika Ipasavyo ni Lazima Wawakilishi wa Wananchi katika Nafasi Zao Kujitoa na Kushirikiana Nao katika Masuala Mbalimbali katika Jamii waliopo Kulingana na Changamoto Zao.

“Kwa Mfano Mimi Katika Ahadi Zangu Niliahidi Kuboresha Vifaa vya Ofisi za Jumuiya na Kushirikiana Nao katika Shughuli Mbalimbali Hadi Sasa Mikoa 15 nimetoa Fotokopi Mashine na Mikoa 17 Nimetoa Kompyuta na Printa Zake Tanzania Visiwani (Zanzibar) Nimeshakamilisha Ahadi Hiyo kwa Mikoa Yote ya Unguja na Pemba Lakini Pia Kwa Kuwa Zanzibar Ndiko Ninapotokea katika Wilaya 12 Zote Nimetoa Vifaa Hivyo kwa Ajili ya Utendaji Kazi Bora;

“Kwa Minajili Hiyo Kama Ulivyoona Leo Nimetoa Hapa Kompyuta mkoani Arusha,Nimemaliza Nchi Nzima,Kwa Sasa Natazamia katika Suala la Elimu Mfano Jana Tulienda wilayani Arumeru Kichama Meru Kuangalia Majengo ya Shule Yetu ya Wazazi ya Sekondari ya Leguruki Kuna Ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi Wenzangu Niliokwenda Nao Wametoa Mifuko Takribani Mia Tatu Mimi Nimeahidi Kutoa Bati 100 kwa Ajili ya Kuezekea Mabweni Hayo” Alisema Giga.

Akizungumzia Hamasa ya Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa CCM na Jumuiya Zake Kujitolea Kusaidia Chama ,Mbunge Giga, Alisema Kuwa Kwa Sasa Wadau Wanatoa Michango Yao Kutokana na Imani Yao kwa Serikali Iliyo Chini ya Mwenyekiti wa Chama Hicho Taifa na Rais Dk.John Joseph Pombe Magufuli, Uongozi wake Umenyooka Akisema Atatekeleza Jambo Fulani Basi Huwa Kweli Maana Wananchi Wana Imani na CCM.

Akizungumza Kwa Niaba ya Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM,Katibu Mkuu,Erasto Sima, Alimpongeza Mbunge Kwa Mchango Wake Mkubwa Anaoufanya katika Jumuiya Hiyo.

“Mimi Nimpongeze Sana Mh. Mbunge Giga Kwa Mchango Wake Mkubwa Kwa Jumuiya Yetu ya Wazazi Kila Mtu ni Shahidi Kwa Haya Uyafanyayo,Kiongozi Akiomba Nafasi Anapaswa Aitumikie Taasisi au Jumuiya Husika Siyo Yeye Atumikiwe Huyo Atakuwa Hatoshi” Alisema Sima.