Home Mchanganyiko TAKUKURU YATOA TAHADHARI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2019

TAKUKURU YATOA TAHADHARI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2019

0

Mkuu wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa mbalimbali kutoka Ofisini kwake TAKUKURU

………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkuu wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo,amesema kuwa katika  kuelekea kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa imeelezwa kuwa Kata, Mitaaa na Vijiji zimekuwa zikiongoza kwa rushwa kwa asilimia 39.4 zikifuatiwa na Ardhi kwa asilimia 13.5 na Elimu  asilimia 12.3 .

Hayo ameyasema leo Ofisini kwake jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa tuhumna zingine zilizobaki zinahusu sekta ya Afya,Uhamiaji,Tarura na vyama vya siasa

Aidha amesema kuwa tuhuma nyingine za rushwa ni katika maeneo ya Mahakama kwa asilimia 7.7 ,Wizara asilimia 5.8,Polisi asilimia 5.2,Sekta binafsi asilimia 5.2 pamoja na Maji asilimia 4.5,hii yote ni katika kipindi cha robo ya Julai hadi septemba 2019 ambapo zilipokelewa jumla ya tuhuma  155.

“Tumekamilisha majalada 15 ya uchunguzi na kufungua mashauri 8 mahakamani ambayo washitakiwa ni watu binafsi na watumishi wa sekta za Elimu,Kilimo,Nida,Tanroads,Watendaji wa Kata na Vijiji na Askari wa Jeshi la Akiba,pia kuna mashauri 34 yanaendelea mahakamani”alisema.

Wakati huohuo katika eneo la kuzuia rushwa Kibwengo amesema kuwa wamefatilia miradi 39 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bil. 46 katika sekta ya ujenzi wa miundombinu,elimu,maji,afya na kilimo.

“Tumebaini viashiria vya ukiukwaji wa taratibu kwenye utekelezaji wa miradi minne yenye thamani ya zaidi ya bil. 1 na hivyo tumeanzisha uchunguzi kuona iwapo kuna vitendo vya rushwa”alisema.

Kibwengo amesema kuwa AKUKURU imeingilia kati utekelezaji wa mkataba wa uundwaji wa kampuni kati ya halmashauri moja na taasisi binafsi kwaajili ya kununua maeneo,kuyapima na kuuza viwanja mkataba ambao ungeweza kuisababishia halamashauri hiyo hasara ya zaidi ya sh.mil 700 kwani baadhi ya taratibu hazikufuatwa na kuelekeza taratibu zifuatwe kabla ya kuendelea na mchakato huo.

Hata hivyo amesema kuwa walifanya uchambuzi wa mifumo miwili ya ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na manunuzi ya umma na kufuatilia utekelezajiwa maazimio ya warsha za mianya ya rushwa katika matumizi ya mashine za EFDs na POS na kubaini kuwa bado kuna wafanyakazi wengi hawatoi risiti wanapotoa huduma na kupoteza mapato.

Ameeleza kuwa  wamemkamata Emmanuel Mziwanda mwenye umri wa miaka 62 ambaye alikuwa  Afisa afya  Mkuu na Mratibu wa mradi wa Belgian Fund for Food Security (BFFS) wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambaye amekuwa akitafutwa tangu julai 2017 anayekabiliwa na mashtaka ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri na kuisababishia serikali hasara ya sh. mil.15.

“Ushahidi wetu unaonyesha alijipatia kwa njia ya udanganyifu,na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake baada ya taratibu za kisheria kukamilika”alisema.

Hata hivyo Kibwengo alisema kuwa TAKUKURU imefungua ofisi wilayani Chemba na hivyo kufanya wilaya zote za mkoa wa Dodoma kuwa na ofisi.

“Hatua hiyo itaboresha juhudio za mapambano dhidi ya rushwa na tunawaomba wakazi wa wilaya hiyo kuitumia ofisi hiyo kwa ukamilifu”amefafanua Kibwengo