Home Biashara TANGA CEMENT: KUFUNGULIWA KWA RELI YA KATI KILIMANJARO-ARUSHA KUMEONGEZA USAMBAZAJI WA SARUJI...

TANGA CEMENT: KUFUNGULIWA KWA RELI YA KATI KILIMANJARO-ARUSHA KUMEONGEZA USAMBAZAJI WA SARUJI YETU

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea katika kiwanda hicho mwishoni mwa wiki iliyopita ili kujionea shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto  katika shughuli nzima ya uzalishaji wa Saruji kiwandani hapo.

…………………………………………….

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart amesema kufufuliwa tena kwa njia ya treni ya Shirika la Reli TRC mikoa ya Kilimanjaro na Arusha  kumesaidia kiwanda hicho kuongeza usambazaji wa saruji katika mikoa hiyo.

Bw.Reinhardt Swart amesema hayo wakati  akizungumza na Wahariri wa Vyombo  mbalimbali vya habari pamoja na waandishi waliotembelea katika kiwanda hicho mwishoni mwa wiki iliyopita ili kujionea shughuli mbalimbali pamoja na changamoto  katika shughuli nzima ya uzalishaji wa Saruji kiwandani hapo.

Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa kiwanda hicho  kinasafirisha saruji kwenda Kilimanjaro na Arusha mabehewa 40 kwa wiki yenye uwezo wa kubeba tani 40 kila moja hivyo unaweza kuona ni kwa kiasi gani tumeongeza usambazaji ukilinganisha na hapo awali  tulipokuwa tukitumia maroli ambayo uwezo wake wa kubeba mzigo ni kidogo na inabidi yawe mengi ili kubeba mzigo kubwa.

Ameongeza kuwa kutokana na hilo ni wazi hata gharama za usafirishaji zinapungua kwa sababu hatulazimiki kutumia maroli mengi kwa sasa kwani mabehewa ya treni yanaweza kubeba mzigo mkubwa zadi.

Hata hivyo ameongeza kwamba bado wanahitaji mabehewa zaidi kutoka Shirika la Reli TRC ili kuongeza mzigo mkubwa zaidi katika usambazaji wa Saruji kwenye  vituo vyao mbalimbali vilivyopo nchini.

Ameongeza kuwa Kiwanda cha Sariji cha Tanga Cement kiliingia mkataba na Shirika la Reli Tanzania TRC ili kusafirisha kiasi cha tani 35.000 kwa mwezi ambapo kiwanda hicho  kimeweka maghala yake katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Tabora, Shinyanga na Mwanza.

Lakini pia kiwanda hichi kina maghala mengine katika mkoa wa Iringa kule  Makambako kuna mpango wa kuongeza  maghala mengine katika mkoa wa Kigoma ili kuongeza zaidi usambazaji wa saruji.

Lengo kubwa na kuhakikisha tunawafikia wateja wetu nchini kote ili kukidhi ushindani wa soko lakini kubwa zaidi kuwahudumia wateja wetu katika kiwango kikubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea kwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Baadhi ya wahariri  wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart wakati alipokuwa akizungumza.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali na waandishi wa habari wakiandika mambo muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart wakati akizungumza nao.

Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa  wa Kiwanda cha Tanga Cement wakiwa katika kikao hicho kilichokutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart.

Baadhi ya waandishi kutoka mkoani Tanga wakishiriki kikao hicho.

 Baadhi ya waandishi kutoka mkoani Tanga na Dar es salaam wakifuatilia kikao hicho.

Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Tanga Cement Bi. Diana Malambugi akitoa mada kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika kikao hicho.

Injinia Gadiel Benjamin wa Kiwanda cha Tanga Cement  akionesha sampuli za udongo na madini ya aina ya Limestone yanayotumika kutengenezea Saruji. katika kiwanda hicho wakati alipotoa mada kuhusu uzalishaji wa Saruji.

Injinia Gadiel Benjamin wa kiwanda cha Tanga Cement akifafanua jambo wakati alipokuwa akielezea namna madini hayo yanavyochakatwa mpaka kufikia viwango vya kutengeneza saruji.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Kiwanda cha Tanga Cement Bi. Nuru Mtanga akifafanua jambo na kuwashukuru wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kutokana na jinsi wanavyotoa ushirikiano kwa kiwanda hicho.

Hili ni eneo ambalo madini ya Limestone yanachimbwa tayari kwa kuchakatwa na kisha kutumika kiwandani kutengeneza Saruji.

Huu ni mtambo wa kuchakata mawe kwa ajili ya kutimika kutengeneza saruji kiwandani.

Moja ya kinu  kinachozalisha saruji

Moja wapo ya vinu vinavyzalisha saruji kiwandani hapo ambacho  kimepumzishwa kwa muda  ili kufanyika matengenezo madogo ya kawaida tayari kwa kuendelea na uzalishaji.

Logolieki Mollel Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Tanga Cement akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari hawapo pichani wakati walipotembelea kiwandani hapo.

 Kinu kipya kikiendelea na uzalishaji wa Saruji kiwandani hapo.