Balozi wa amani Bw toshiaki sasada akiwa pamoja na kiongozi wa taifa wa family Federation Mch. Stylos Simbamwene
Mabalozi wa amani wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa family Federation katika uwanja wa ndege
Wanachama federation wakicheza kwa furaha katika uwanja ndege
………………………….
Na. Stahmil Mohamed.
Jumla ya mabalozi wa amani ya Dunia 41 wamewasili nchini kwa ajili ya tamasha la amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabalozi hao Wa Amani wamewasili kutokea japan na maeneo mengine ya nchi hiyo kuhudhuria tamasha la amani ya Dunia linalolenga kukutanisha wanandoa, wajane pamoja watu mbalimbali kuendelea kuenzi amani pamoja na kufundisha maadili ili kujenga kizazi chenye uzalendo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mapokezi hayo katika uwanja Mpya Wa ndege kiongozi wa taifa wa taasisi hiyo Stylos Leo Simbamwene amesema kuwa wageni hao ni Mabalozi Wa Wa Amani wanamuenzi muasisi wa amani Baba moon kwa kutoa mafundisho ya maadili pamoja na amani ili duniani kuwepo na upendo, furaha,na ushirikiano .
Simbamwene amesema kuwa ujio huu ni watatu kutoka kwa mabalozi hao ambapo mara ya kwanza walianza Mbeya kisha Arusha na sasa ni zamu ya Dar es salaam na baada ya hapo wataenda mkoani morogoro ambapo napo kutafanyika tamasha la amani hasa kwa upande wa wanawake.
Simbamwene amesema mbali na tamasha hilo mabalozi hao wa amani watatembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa kutembelea mbuga za wanyama hasa Mikumi.
Hata hivyo Simbamwene ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha watanzania na kusema kuwa kumeibuka wimbi kubwa la matapeli wanaotumia jina la taasisi hiyo kutapeli watu kwa kuwalipisha ghalama za kujiunga na taasisi hiyo ya amani na kusema kuwa ni kinyume na taasisi yao kwani wao hawana utaratibu wa kuwalipisha ghalama zozote za kujiunga na taasisi hiyo hivyo watanzania watoe ushirikiano kuhakikisha wanatoa taarifa ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi hao wa amani Bw.Toshiaki Sasada Amesema kuwa wamefurahi kuja kwa mara nyengine Tanzania katika tamasha hilo kwa ajili ya kujenga kizazi cha uzalendo pia amefurahi kutua katika uwanja mpya wa ndege na kusema kuwa Tanzania inapiga hatua katika maendeleo na amechukua fursa hiyo kumpongeza Rais Wa Jamhuri wa muungano wa wa Tanzania John pombe Magufuli kwa jitihada mbalimbali anazozifanya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua katika masuala mbalimbali ya Maendeleo