Home Michezo LUKAKU ANG’ARA,INTER MILANI IKIPATA USHINDI DHIDI YA LECCE

LUKAKU ANG’ARA,INTER MILANI IKIPATA USHINDI DHIDI YA LECCE

0

************

NA EMMANUEL MBATILO

Mshambuliaji mpya Wa Inter Milan Romelu Lukaku ameanza kuishambulia ligi kuu ya Italia Serie A akifunga bao 1 katika ushindi Wa bao 4-0 walioupata usiku Wa Jana dhidi ya Lecce katika uwanja Wa San Siro.

Lukaku ambaye hakuweza kuwashawishi matajiri wa klabu ya Manchester United na baadae kuamua kutimkia Seria A katika Klabu ya Inter Milan hivyo jana kuwaonesha miamba hiyo ya Italia hawakukosea kuchukua saini ya mshambuliaji huyo mwenye asili ya Congo anaeichezea timu ya taifa ya Ubeligiji.

Lukaku alifunga bao hilo Dakika ya 60 ikiwa ni bao la 3 la Inter Milan katika mchezo huo bao ambalo lilimfanya apongezwe na kocha wake Antonio Conte hasa baada ya kuhangaika sana katika usajili wake kutoka Manchester United mwezi uliopita.