Zaidi ya wafanyabiashara na wajasiriamali 1000 wanatarajia kuanza kunifaika na mradi wa soko kubwa lenye hadhi ya kimataifa linalojengwa mkoani Njombe na kampuni ya NADRA Engeneering and Construction Com.ltd katika halmashauri ya mji wa Njombe .
Soko hilo la ghorofa linajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia huku kiasi cha zaidi ya bil 9.3 kitatumika kukamilisha mradi huo ulioanza kujengwa mwezi januari mwaka huu na kutakiwa kukamilika octoba.
Edwin Mwanzinga ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe anasema serikali inategemea kuongeza mapato pindi soko litakapo anza kutumika kutoka kukusanya mil 3 katika soko lililovunjwa hadi kufikia kadilio la makusanyo ya mil 20 kila mwezi kwa soko jipya.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amewatoa shaka wafanyabiashara kuondoa shaka kuhusu gharama za kodi ya milango pamoja na meza kwa kuwa halmashauri imedhamilia kuweka bei rafiki kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo na kuwataka kuwa subira na ujenzi unaoendelea.
Wakati walengwa wa mradi huo wakiomba kuharakisha ujenzi ili kuwarejesha wafanyabiashara waliopisha ujenzi nae Mkandarasi wa mradi kutoka kampuni ya NANDRA Engeneering and Constraction Ltd Justin Mboka anasema mradi umefikia asilimia 75 na wanatarajia kukabidhi serikalini ifikapo mwezi octoba mwaka huu nakueleza sababu ya kuomba muda wa nyongeza ili kukamilisha mradi.
Katika hatua nyingine mkandarasi huyo amezitaja sababu za kuomba kuongezewa muda wa ziada ili kukamilisha mradi huo uliokuwa ukamilike mwezi wa nane na badala yake utakabidhiwa mwezi Octoba ambapo amesema hali ya hewa ya mvua kubwa,ukosefu wa materials za zege pamoja na changamoto ya kuhamisha mnara uliokuwepo eneo la ujenzi wa soko ambapo zimesababisha kuchelewa zaidi ya mwezi mmoja.