Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihtubia mbele ya mgeni wake Rais wa Jamhuriya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuriya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam huku mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yaWafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakisalimiana mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiasharawahao.
………………………………………………………..
Rais Magufuli, amesema hakuna uchaguzi mwingine katika kuhakikisha Afrika inaondokana na unyonge zaidi ya kuungana katika mapambano ya kiuchumi.
Rais Magufuli amesema “Udugu na muungano wetu utakuwa hauna maana ikiwa tutashindwa kufikia lengo hili la kukua kiuchumi. Tuendelee kuwa pamoja kwa sababau historia yetu inafanana,” .
Rais Dk. John Magufuli amesema hayo akiwa na mgeni wake Rais Cyril Ramaphosa wakati wa jukwa la baishara kati ya wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika Kusini na Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo ambapo amesisitiza kuwa hakuna kinacheweza kuzuia Afrika kuwa na maendeleo.
Rais Magufuli alisema, zaidia ya asilimia 70 ya uzalishaji katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) bidhaa zinakwenda Afrika Kusini. Alisisitiza, bidhaa nyingi zinakwenda Afrika Kusini ikiwemo mbogamboga na matunda, nafaka, vinywaji, mpira na huduma za usafiri.
Rais Magufuli amebainisha kuwa , Afrika Kusini ni nchi ya pili kwa uwekezaji nchini ambapo kwa mwaka jana 2018 mauzo katika biashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 5.3,” alisema.
“Sekta ya viwanda inazidi kuongeza urafiki huu, hata hivyo uzalisihaji wetu katika taifa la Tanzania bado uko chini. Kama taifa tunaamini tunahuisha uwekezaji wa viwanda ambavyo vinaongeza thamani katika bidhaa zetu ambazo zinasafirishwa zikiwa ghafi na kupunguza bidhaa kutoka Ulaya,” ameongeza:
“Afrika Kusini ni ya 13 kwa uwekezaji nchini, takwimu zinaonyesha uhusiano wetu katika uchumi ni mkubwa, maendeleo haya yanaonyesha urafiki wetu wa kibiashara, kiuchumi, kijamii na kisiasa unaimarisha uwekezaji huu.
“Tanzania ni ya pili kwa idadi ya mifugo baada ya Ethiopia barani Afrika, tunahitaji kutumia vema fursa hii kuchakata mazao ya mifugo, vilevile kutumia bidhaa zitokanazo na samaki kutoka kwenye bahari, mito na mabwawa. Lengo la msingi ni kuwa na bidhaa zetu na kuacha kusafirisha bidhaa ghafi ambapo pia tutakuwa tunasafirisha ajira.”
Hivyo, amemuasa Rais Ramaphosa kutumia fursa hiyo kuleta wawekezaji katika viwanda vya dawa na vifaa tiba.
“Niwakumbushe kitu kimoja tu, katika sekta ya utalii ni eneo zuri kwa uwekezaji nchini, Tanzania ni ya pili kwa ukubwa katika utalii duniani. Tunazidi kuongeza mbuga za taifa, tunawekeza katika hoteli, kambi za kupumzika na utalii wa kihistoria. Nawaomba mkipata muda mtembelee vivutio vyetu si kwa kujifurahisha tu lakini pia kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji,” alisema.
Rais Magufuli amekuwa mkali kwa watu wanaosambaza uongo kuwa Tanzania si sehemu salama kwa wawekezaji. Amesema huo ni uongo unapasa kupuuzwa kwani Tanzania inasifika kwa amani na utulivu wa kisiasa.
Rais Ramaphosa amesema “Mlitufunza, mlituunga mkono kwa njia nyingi na kutusaidia kiasi kikubwa, tunashukuru kwa dhati. Hii ndio sababu muunganiko wetu si wa kihistoria tu bali wa damu. Kujitoa kwenu muhanga na kutuunga mkono katika mapambano ndio maana leo Afrika Kusini imekuwa huru,” alisema.
Rais Cyril Ramaphosa alisema ameongeza kuwa Tanzania na Afrika Kusini ina urafiki wa miaka mingi, hakuna maneno ya kueleza kwa namna ilivyowasaidia wakati wa kuhangaika, wakati wa kipindi kigumu.
“Afrika katika miaka ijayo itakuwa na idadi kubwa ya watu hadi kufikia bilioni moja, mahitaji yataongezeka vilevile. Mahitaji ya kijamii pia yataongezeka kwa kila raia”.Amesema Rais Ramaphosa.
Jamii ya wafanyabiashar Afrika Kusini wanafikia asilimia 70, maana yake fursa hii hatutaiacha. Tuna kampuni zaidi ya 208 hapa Tanzania ambapo kuna waajiriwa zaidi ya 21,000.
“Huu ndio wakati wa kuimarisha viwanda na uwekezaji, inawezekana tulifanikiwa kuondoa changamoto tulizokuwa nazo awali, lakini ili kufanya hivyo lazima tuondoe vikwanzo katika ufanyaji biashara.
Jambo kubwa kwa waafrika ni kuendeleza uchumi wa ndani ambao unasaidia kukuza biashara, bara la Afrika lina changamoto nyingi lakini fursa zilizopo ni nyingi pia. Tunaiona Afrika kama bara linalokua kwa kasi na sisi tupo tayari, kwa kuwa sisi ndio tutakaokuwa wa kwanza kukuza na kuliongoza bara hili, lazima tuwe tayari kwa mabadiliko haya.