Watanzania wameombwa kuwekeza kibiashara katika nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC na kutohofia suala usalama kwa sababu serikali inajitahidi kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani pamoja na changamoto za kiusalama zinazojitokeza eneo la mashariki wa DRC .
Hayo yamesemwa na balozi wa Kongo nchini Tanzania Luteni Jenerali (staafu) Paul.I.Mella wakati alipokuwa anaongea katika mkutano na wafanyabiashara mkoani Kagera ambao umekutanisha wafanyabiashara wa kutoka katika nchi za Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aidha amesema kuwa nchi zetu zinatakiwa kuwa na masoko ya mipakani ili kuwepo kwa fursa baina ya pande mbili ili kujenga ushirikiano kwa wafanyabiasha wa nchi zote.
Mkutano huo umehudhuriwa na mabalozi wa Tanzania kutoka nchi za Uganda, Rwanda, na Burundi sambamba na mkuu wa mkoa wa Kagera mh.Brigedia Jeneral Marko Gaguti pamoja makatibu tawala wilaya wa mkoa wa Kagera Balozi Israel Kumuzora.
Naye balozi wa Uganda Mh. Aziz.P. Mlima ‘ameeleza fursa zinazo patikana nchini Uganda na kutazitaja bidhaa zinazokuza soko nchini Uganda kuwa ni Maparachichi na bidhaa nyingine. Hata hivyo amaeleza fursa za elimu kwa upande wa nchi ya Uganda kuwa ada ya elimu ya uganda ni nafuu zaidi ukilinganisha na maeneo mengine.