Home Mchanganyiko WANAOSAMBAZA PICHA ZA MAREHEMU KUCHUKURIWA HATUA

WANAOSAMBAZA PICHA ZA MAREHEMU KUCHUKURIWA HATUA

0

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh  Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuwakamata na kuwachukulia sheria wale wote wanaosambaza picha za marehemu katika mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo nikosa kisheria 

Mh Masauni ametoa kauli hiyo jana Ogosti 12 mjini Morogoro mara baada ya swala ya Eid iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Boma lord,ambapo amesema kuwa kusambaza picha za marehemu katika mitandao ya kijamii ni kuwadhalilisha wahusika na ni uvunjaji wa sheria za nchi.

“Ninaziagiza mamlaka na vyombo vinavyohusika vihakikishe vinafuatilia na kuchukua hatua kwa wale ambao wanakiuka sheria za nchi yetu kwa kusambaza mitandaoni picha za marehemu,” aliagiza Mh Masauni.

Aidha Mh Masauni amesema siyo vema kuanza kutumia majanga ya kitaifa kama ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro na kusababisha  watu zaidi ya 70 kufariki dunia ndani ya muda mfupi.hivyo kuanza kusambaza picha za waathirika mitandaoni kwa dhamira ya kudhalilisha. 

Sio jambo la busala.

“Watu hawa wamefariki dunia na mtu yeyote katika tukio lile angekufa, mimi au wewe, ndugu yako au jamaa yako, fikiria kama ni jambo limekukuta au ndugu yako halafu ukachukua picha na kuisambaza kwenye mitandao, katika mazingira kama yale,” Masauni alisema.