Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Bohari ya Dawa(MSD) kwa wepesi na uharaka wa kufikisha dawa na vifaa tiba mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi wa janga la moto lililotokea jana mkoani humo.
MSD imeweza kufikisha dawa na vifaa walivyoomba huku timu ya MSD inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Laurean Bwanakunu ikiendelea kuwa karibu na wataalamu wa afya mkoani humo kwa ajili ya kutoa ushirikiano pale inapohitajika.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu anaongoza timu ya Wizara hiyo, ikiwa na viongozi wakuu ambao ni Katibu Mkuu wa Afya Dkt. Zainab Chaula na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Prof. Mohamed Kambi wanaofuatilia kwa karibu huduma na mahitaji yote yanayohitajika kwa majeruhi wa janga hilo la moto mkoani Morogoro.
Hadi Sasa dawa na vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 200 zimeishapelekwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Timu zote hizi ziko karibu na ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa kinachoongozwa waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Walemavu, Vijana na Bunge. na Mhe. Jenister Mhagama.