Home Uncategorized MAJALIWA AWAJULIA HALI MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA LORI LA MAFUTA...

MAJALIWA AWAJULIA HALI MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA LORI LA MAFUTA LILILOPINDUKA MOROGORO NA KUSHIRIKI IBADA YA KUWAOMBEA MAREHEMU

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole , Shukuru Fabian ambye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali, Hans Kifah ambaye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)