************
NJOMBE
Wanufaika wa mpando wa kunusuru kaya masikini Tanzania TASAFI katika vitongoji sita vya kijiji cha Wanginyi wilayani Njombe wamemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwapa uafafanuzi kwa nini hawajapatiwa fedha hizo tangu mwaka huu umeanza ili hali maeneo mengine yameendelea kunufaika na mpango huo.
Wakizumza katika mkutano wa hadhara mbele ya mbunge wa Jimbo la Lupembe Joram Hongoli wanufaika hao akiwemo Mzee Samuel Ngimbuchi wamesema hali yao imezidi kuwa ngumu kwa kuwa idadi kubwa ya wazee na familia duni zimemekuwa zikitegemea fedha hiyo kuendeleza miradi ya ufugaji na kilimo pamoja na maisha yao ya kila siku hivyo wanaiomba serikali kuiona changamoto hiyo na kuitafutia majibu.
Katika hatua nyingine wakazi hao wameonekana kukosoa utaratibu uliotumika awali kuainisha kaya zenye uhitaji wa mfuko kwa kuwa wazee wengi wenye sifa pamoja na kaya duni zimeachwa huku baadhi wasio nasifa wakionekana kunufaika na mpango jambo ambalo wanaona lilitawaliwa na upendeleo na kuiomba serikali kuanzisha tena mchakato wa usajiri wa wahitaji.
Kuhusu malalamiko ya kutawaliwa kwa upendeleo wakati zoezi la uandikishaji linafanyika , mwenyekiti wa kijiji cha Wanginyi Emmanuel Mwenda anakanusha tuhuma hizo kwa waratibu wa tasaf huku akidai idadi kubwa ya watu wenye sifa walikuwa wanatoa taarifa za uongo wakati wakukusanya taarifa za watu wenye sifa za kunufaika na mpango wa TASAFU hatua ambayo imekuwa tatizo hivi sasa.
Baada ya kumalizika kwa mkutano Fullshangwe imezungumza mwakilishi wa mkurugenzi katika mkutano huo Steven Vidoga ambaye anasema hakuna kijiji ambacho kimeachwa katika malipo bali serikali katika hatua za mwisho za kukamilisha taarifa za awamu ya mpango ili kuanza kutoa fedha na miradi kwa wanufaika.
Kijiji cha wanginyi kinawakazi zaidi ya elfu moja kina idadi kubwa ya wazee na kaya zenye maisha duni lakini wanufaika 58 pekee ndiyo wanapata fedha za tasaf.