Home Biashara SERIKALI YAPONGEZWA MFUMO WA GePG

SERIKALI YAPONGEZWA MFUMO WA GePG

0

Mwaandishi Mashughuri wa Vitabu Nchini Tanzania, Bw. Richard Mabala (kushoto), akipata maelezo kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki- GePG, kutoka kwa mtaalam wa mfumo huo wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Stella Nguma, alipotembelea katika banda la Wizara hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane eneo la Nyakabindi Mkoani Simiyu

Waataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (kushoto), wakitoa elimu ya masuala ya Bajeti, Sera, Pensheni na Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki- GePG, katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Wanafunzi wa Kidato cha Tatu kutoka Sekondari ya Biashara Mkoani Simiyu, Happiness Gwalugwa na Elen Mhuly, wakipata maelezo kuhusu Masuala ya Bajeti kutoka kwa Mtaalamu wa Bajeti Bw. Asajile Mwaipopo, walipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Mkazi wa Bariadi Mkoani Simiyu Bi. Mariamu Ezekieli, akielezwa namna bajeti inavyoandaliwa na umuhimu wake kwa wakulima, kutoka kwa mtaalamu wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Asajile Mwaipopo, alipotembelea banda la Wizara hiyo, katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Muonekano wa Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango- Simiyu)

***************

Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu

Mwandishi Mashughuli wa Vitabu nchini kikiwemo cha “Mabala The Farm”, Bw. Richard Mabala, ameipongeza Serikali kwa kubuni mfumo wa kielektroniki wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali- GePG kwa kuwa unasaidia kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma na kuweka uwazi wa mapato na matumizi.

Alibainisha hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Alisema kuwa Mfumo wa GePG unamanufaa kwa Serikali na wananchi, kutokana na uwazi uliopo lakini pia makusanyo kufika kwa wakati katika maeneo husika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na mengine.

“Mfumo huo utanisaidia malipo ya kodi ya majengo na kodi nyingine kwa kuwa unaondoa urasimu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya malipo na pia unaokoa muda kwa kuwa ni rahisi kuutumia kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Bw. Mabala.

Mwandishi huyo wa Vitabu ametoa wito kwa wadau, ikiwemo Serikali kuhamasisha matumizi ya Simu zenye uwezo wa kutumia mfumo wa GePG, hasa katika maeneo ya vijijini ambako idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wakulima wanapatikana.

Tanzania inaidadi kubwa ya vijana ambao wanauwezo wa kutumia mfumo wa kielektroniki katika malipo ya Serikali ukilinganisha na wazee, hivyo umekuja wakati mwafaka na utakua na nafasi kubwa ya kuchochea maendeleleo ya kiuchumi.

Bw. Mabala amesema kuwa, Mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika Mipango ya Serikali ukilinganisha na awali ambapo mfumo huo haukuwepo hivyo uwepo wa GePG utaongeza ufanisi kiutendaji na kuharakisha maendeleo kulingana na ushindani uliopo katika nyanja mbalimbali duniani hasa katika mifumo ya teknolojia.

Kwa upande wao wanafunzi wa Sekondari ya Biashara iliyopo Bariadi Mkoani Simiyu, wameipongeza Serikali kwa kutumia mfumo wa kisasa wa GePG, hivyo elimu waliyoipata katika maonesho ya Nanenane wataipeleka kwa wazazi wao na jamii inayowazunguka ili waweze kuitumia katika malipo ya Serikali.