Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na baadhi ya viongozi na wananchi wakifanya usafi katika maeneo ya Uwanja wa ndege
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Paul Makonda akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya Usafi uliofanyika kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
*********
NA EMMANUEL MBATILO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewataka watumishi wa Umma wajiwekee utamaduni wa ufanyaji usafi katika maeneo yao ya kazi pasipokusubiri mpaka kusimamiwa ama kuambiwa na viongozi wa juu.
Ameyasema hayo leo baada ya kuzindua kampeni ya ufanyaji usafi kwa Jiji la Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa SADC utaofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wageni takribani 1000.
Aidha Mh.Makonda ameendelea kusisitiza zaidi suala la usafi hasa kwa wananchi wote waishio Mkoa wa Dar es Salaam na wote wanaoingia kufanya biashara mbalimbali au kwa ajili ya utalii wa aina yoyote ile kuhakikisha wanazingatia suala la usafi wao kuanzia katika muonekano mzima na mahali kote watakapokua.
“Mtakae mkamata akichafua mazingira mnatakiwa kumpatia adhabu ya kudeki barabara kipande kama kilomita 1 ama zaidi ili iwe fundisho kwa wengine. Mtu mwenye gari mkimkamata msimtoze pesa, pesa anayo atakulipa tena kwa kiburi na kuondoka”. Amesema Mh.Makonda.
Hata hivyo Mh.Makonda amesema kuwa Wanaokaa kando ya barabara kuu amewataka kuhakikisha wanafanya usafi katika makazi yao hivyo kufikia tarehe 5 mwezi Agosti Jiji la Dar es Salaam liwe safi
“Matumaini yangu miti yote itakayopandwa lazima ikuwe, watu wote wa mazingira kwa kila wilaya miti hiyo itakayopandwa ikifa andika na barua yako ya kuacha kazi aiwezekani kila mwaka tunatenga bajeti ya upandaji wa miti”. Amesema Mh.Makonda.
Amewapa pongezi wamiliki wa daladala jijini Dar es Salaam kuwa na chombo cha kuwekea taka katika daladala zao kuendana na kampeni ya usafi kwa jiji la Dar es Salaam