***********
NA EMMANUEL MBATILO
Kumekuwa na ongezeko la idadi ya vyuo katika maonesho ya 14 ya elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hasa kwa kipindi hiki vyuo kutoka nje ya nchi kushiriki maonesho hayo na kutangaza fursa zilizopo kwenye vyuo vyao.
Akizungumza na Fullshangwe blog katika Maonesho hayo Naibu Makamu Mkuu Tafiti na Maarifa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Cuthbert Kimambo amesema kuwa katika banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi watarajiwa wamefika kwa wingi pamoja na wazazi wao kwaajili ya kuangalia utaratibu wa kuweza kujiunga na Chuo hicho.
Aidha,Prof.Kimambo amesema kuwa amefurahi kuona vyuo vikuu vya nje kushiriki maonesho hayo hivyo wanawashawishi na wao kufanya hivyo kutangaza chuo hicho hivyo kutawapa fursa kutafuta wanafunzi nje ya nchi ili kuweza kuongeza idadi ya wanafunzi wa kimataifa.
“Maonesho ya sasa yamekuwa tofauti, wanafunzi watarajiwa wameweza kuhudhulia kwa wingi katika maonesho haya pamoja na idadi ya kubwa ya Vyuo mbalimbali kwa kipindi hiki wameweza kuhudhulia kwaajili ya kutangaza fursa zilizopo kwenye vyuo vyao”. Amesema Prof.Kimambo
Upande wa Wanafunzi walifika katika maonesho hayo wamesema kuwa uwepo wa vyuo vingi katika maonesho hayo kutachangia kupata fursa ya kuchagua vyuo ambavyo vinawafaa kutegemeana na program ambazo wanazitoa vyuo hivyo.