Home Michezo CAF yarekebisha tarehe za kufuzu AFCON 2021

CAF yarekebisha tarehe za kufuzu AFCON 2021

0

*************

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kikao chake kilichokaa Julai 17,2019 kimefanya marekebisho ya michezo ya kufuzu Fainali za Afrika (AFCON) 2021.
Hatua ya awali kufuzu itachezwa kati ya Oktoba 7-15,2019 wakati michezo mingine itakua kati ya Novemba 11-19,2019.
Michezo inayofuata itachezwa kati ya Agosti 31,2020 na Septemba 8,2020 na hatua inayofuata kuchezwa kati ya Oktoba 3-15,2020.
Michezo ya kumalizia itachezwa kati ya Novemba 9-17,2020.