Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mh.Damas Ndumbalo akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta binafsi pamoja na wanahabari katika mkutano wa ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Uganda utakofanyika Septemba 3 hadi 5 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta binafsi pamoja na wanahabari katika mkutano wa ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Uganda utakofanyika Septemba 3 hadi 5 Jijini Dar es Salaam
****************
NA EMMANUEL MBATILO
Watanzania watakiwa kushirikiana kwa pamoja kutafuta masoko ya kibiashara nchini Uganda kupitia mkutano wa Kwanza wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili utakaofanyika Septemba 3 hadi 5 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mkutano huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mh.Damas Ndumbalo amesema kuwa Serikali ya Tanzania imejitahidi kutengeneza miundombinu mizuri ya kusaidia kukuza uchumi hasa katika sekta ya kibiashara hapa nchini hivyo watanzania wanatakiwa kutumia fursa kupitia mkutano huo kushirikiana na wafanyabiashara kutoka Uganda.
Aidha Mh.Ndumbalo amewataka watanzania waweze kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo kwani kuteleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini hasa tukishirikiana vizuri na wafanyabiashara kutoka nchini Uganda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye amesema kuwa wao kama wahusika na waandaaji wa mkutano huo wataendelea kushirikiana na serikali kuandaa makongamono ya kutosha na yenye faida hapa nchini.
“Uhusiano kati ya nchi ya Uganda na Tanzania ni mzuri toka zamani na ndo maana tumekuwa tukishirikiana nao katika maendeleo kati ya nchi hizi mbili hivyo tutegemee shule binafsi za Uganda kupata fursa kupata walimu wa kufundisha lugha ya Kiswahili kutoka Tanzania”. Amesema Bw.Sembeye.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Uganda,Dkt Aziz Mlima amesema kuwa kuunganishwa kwa wafanyabiashara wawekezaji waliopo Uganda na Tanzana ni kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara kati ya nchi zote mbili na kuleta maendeleo ya kiuchumi.
“Watanzania na waganda wanatakiwa kujiandaa kutumia fursa zitakazojitokeza katika nkutano huo wa kibiashara”. Amesema Dkt.Mlima.