*******************
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Chama Cha Mpira wa Miguu Songwe (SOREFA) na familia ya aliyekua Katibu wa SOREFA,William Mwamlima aliyefariki leo asubuhi.
Kwa niaba ya TFF,Rais Karia,amesema amepokea taarifa za msiba wa William Mwamlima kwa mshtuko mkubwa.
Rais Karia amesem Marehemu Mwamlima bado mchango wake ulikua ukihitajika katika Mpira wa Miguu Mkoa wa Songwe na kwenye Mpira wa Miguu kiujumla.
Aidha Rais Karia ametoa pole kwa Familia ya Mwamlima,Chama Cha Mpira wa Miguu Songwe,Ndugu,Jamaa na Marafiki.
Mungu ailaze roho ya Marehemu William Mwamlima mahali pema Peponi,Amina