Mkurugenzi wa Kinga Dkt.Leonard Subi kushoto akimfanyia upasuahi mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma ya upasuaji wa mabusha kwenye kliniki hiyo
**************
Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele imefanya uzinduzi wa kiliniki tembezi ya upasuaji wa Mabusha kwa wananchi wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.
Akizindua kliniki hiyo Mkurugenzi wa Kinga Dkt.Leonard Subi amesema mpaka sasa wagonjwa 353 wamekwishapasuliwa na zoezi hilo litaendelea wilayani hapo na baadae kuhamia wilaya Ruangwa. Matarajio ni kufikia wagonjwa 600 Kwa mkoa wa Lindi.
Ugonjwa wa Mabusha na Matende umeathiri zaidi ya watu Milioni 120 Duniani na hapa nchini takribani watu 25,000 wanakadiriwa kuwa na Mabusha au Matende .Ugonjwa huu huathiri sehemu mbalimbali za mwili wengi miguuni au mkononi.