Home Mchanganyiko SERIKALI YA UJERUMANI YAIPIGA JEKI SEKTA YA MAJI

SERIKALI YA UJERUMANI YAIPIGA JEKI SEKTA YA MAJI

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo,akizungumza mara baada ya kusaini  Mkataba wa Euro 6.0 na Serikali ya Ujerumani ambapo fedha hizo zitatumika kuboresha sekta ya maji.

Mkuu wa Programu ya Maji katika Shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) Dr. Johannes Schoeneberger akizungumza baada ya kuingia

Mkataba wa Euro 6.0 ambazo zimetolewa na  Serikali ya Ujerumani ambapo fedha hizo zitatumika kuboresha sekta ya maji.

Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo akiwa na Mkuu wa Programu ya Maji katika Shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) Dr. Johannes Schoeneberger wakiwekeana saini ya Mkataba wa Euro 6.0 milioni na Serikali ya Ujerumani ambapo fedha hizo zitatumika kuboresha sekta ya maji.

Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo na Mkuu wa Programu ya Maji katika Shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ)Dr. Johannes Schoeneberger wakibadilishana fomu mara baada ya kusaini  ya Mkataba wa Euro 6.0 milioni na Serikali ya Ujerumani ambapo fedha hizo zitatumika kuboresha sekta ya maji.

Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuingia mktaba wa Euro 6.0 milioni na Serikali ya Ujerumani ambapo fedha hizo zitatumika kuboresha sekta ya maji.

…………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali ya Ujerumani imetoa  Euro milioni 6.0 kwa ajili ya kusaidia

miradi ya maji nchini ikiwemo kuboresha usambazaji na miundombinu ya maji.

Makubaliano hayo yalisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo na Mkuu wa Programu ya Maji katika Shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) Dr. Johannes Schoeneberger

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Profesa Mkumbo aliwataka watumishi wa wizara hiyo kutekeleza yale yaliyomo katika makabiliano hayo bila visingizio.

“Serikali hii ni Serikali ya matokeo sio mchakato. Kama kununua magari basi tununue magari sio stori ndefu unajua tulishatoa tangazo sijui limeenda wapi tunataka matokeo,”amesema Prof.Mkumbo

Kwa upande wake Dr. Johannes Schoeneberger alisema kuwa fedha hizo si fedha za Serikali ya Ujerumani bali ni fedha za walipakodi wa Ujerumani na hivyo zitumike kuwasaidia walengwa ambao ni Watanzania.

“Matumizi, matokeo, utendaji, uhakikishaji yazingatie kuwa ni

ushirikiano huu unalenga katika kumfikia mwananchi kupitia Wizara