Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti yaUtumishi wa Umma, Dkt Merry Mwanjelwa, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Mapambano dhidi ya Rushwa, Cherity Nchimunya, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.
Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad, akifuatilia mawasilisho ya mtoa mada wakati wa mjadala wa namna ya kupambana na rushwa nchini Tanzania, kongamano lililofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu na shule za sekondari, wakifuatilia mawasilisho ya mtoa mada wakati wa mjadala wa namna ya kupambana na rushwa nchini Tanzania, kongamano lililofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa waandishi wa habari, Blaya Moses Mwandishi kutoka Star Tv( mwenye shati jeupe wa kwanza kushoto, akiwasilisha mawazo ya waandishi wa habari juu ya mapambano dhidi ya rushwa katika kongamano hilo, lililofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, CP Diwani Athumani, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damasi Ndumbaro katikati, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mara baada ya kumalizika kwa kongamano la kujadili maswala ya rushwa, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damasi Ndumbaro katikati, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanya kazi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) mara baada ya kumalizika kwa kongamano la kujadili maswala ya rushwa, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti yaUtumishi wa Umma, Dkt Merry Mwanjelwa, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.Katibu Mtendaji wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Mapambano dhidi ya Rushwa, Cherity Nchimunya, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad, akifuatilia mawasilisho ya mtoa mada wakati wa mjadala wa namna ya kupambana na rushwa nchini Tanzania, kongamano lililofanyika jijini Dodoma.Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu na shule za sekondari, wakifuatilia mawasilisho ya mtoa mada wakati wa mjadala wa namna ya kupambana na rushwa nchini Tanzania, kongamano lililofanyika jijini Dodoma.Mwakilishi wa waandishi wa habari, Blaya Moses Mwandishi kutoka Star Tv( mwenye shati jeupe wa kwanza kushoto, akiwasilisha mawazo ya waandishi wa habari juu ya mapambano dhidi ya rushwa katika kongamano hilo, lililofanyika jijini Dodoma.Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, CP Diwani Athumani, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damasi Ndumbaro katikati, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mara baada ya kumalizika kwa kongamano la kujadili maswala ya rushwa, tukio lililofanyika jijini Dodoma.Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damasi Ndumbaro katikati, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanya kazi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) mara baada ya kumalizika kwa kongamano la kujadili maswala ya rushwa, tukio lililofanyika jijini Dodoma.Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, akifuatilia mawasilisho ya mtoa mada wakati wa mjadala wa namna ya kupambana na rushwa nchini Tanzania, kongamano lililofanyika jijini Dodoma.…………………….Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.SERIKALI imesema imeweka nguvu na msisitizo mkubwa katika kupambana na rushwa, kwani rushwa imekuwa ikirudisha sana juhudi za kupambana na umasikini jikomboa kiuchumi na kupoteza haki za watu wengi katika jamii.Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma, na naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damasi Ndumbaro, wakati akizungumza kwenye kongamano la siku maalumu ya mapambano dhidi rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika(AU).Ambapo umefanyika jijini Dodoma, na kutumia siku hiyo kama ni siku ya kuhamasisha, kuwapa elimu, na kuwajengea uwezo vijana namna ya kupambana na rushwa, ambapo kongamano hilo limehusisha wanafunzi wa vyuo vikuu, na wanafunzi wa sekondari na waandishi wa habari.Dkt Ndumbaro amesema kama nchi wameweka mkazo mkubwa kuhakikisha wanapambana na rushwa, na kwa kuhakikisha hayo yanafanikiwa Tanzania imejiunga na kusaini mikataba na itifaki za kupambana na rushwa kimataifa na kikanda.“Tanzania kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano katika kupambana na rushwa imesaini na kuridhia mikataba na itifaki za kupambana na rushwa kimataifa na kikanda, hii ni pamoja na mikataba ya umoja wa kimataifa wa kupambana na rushwa” amesema dkt Ndumbaro.Ametaja baadhi ya mikataba hiyo ni mkataba wa umoja wa kimataifa wa kupambana na rushwa(UNCAC,2003), itifaki ya nchi za kusini mwa bara la Afrika ya kupambana na rushwa(SADC Protocol Against Corruption, 2001, na mkataba wa mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za afrika(AU Convention on preventing and Combating Corruption, 2003).Nyingine ni mwanachama wa shirikisho la taasisi za mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika(AAACA) jumuiya ya madola(CAACA) pamoja na Afrika mashariki( EAAACA) amesema Tanzania pia ni mwenyeji wa bodi ya umoja Afrika ya ushauri kuhusu maswala ya rushwa ambapo makao makuu yake yapo Arusha.Amesema kwa mkazo huo tafiti zinaonyesha kuongezeka kwa kiwango cha utawala bora kwa kupata asilimia 58.5/100.“Tanzania imeonekana kuongeza kiwango cha utawala bora kwa kupata alama 58.5/100,na kuwa nchi ya kumi na moja11 kati ya nchi 54 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na 2017 ambapo ilipata alama 57.5/100 na kuwa nchi ya 17 katika bara la Afrika kwa mujibu wa Mo Ibrahim Index of African Governance” amesema.Aidha amewataka TAKUKURU kuhakikisha wanafanya kazi kwa uwazi na waminifu ili kukomesha vitendo vya rushwa hapa nchini na kuwa na utawala bora.Kwa upande wake Mkurugenzi wa mkuu wa TAKUKURU CP, Diwani Athumani, amesema wao wamekuwa wakifanya kazi na kuhakikisha wanakomesha vitendo vya rushwa hapa nchini.Amesema wamekuwa wakifanya kazi na kuhakikisha taarifa zinazopatikana zinawafikia wananchi ili waweze kujifunza kuhusu maswala ya rushwa na kuhakikisha mali ambazo hazikupatikana kwa halali zinarudishwa serikalini kwa mujibu wa sheria.Aidha amesema moja ya changamoto ambazo zinaikabili taasisi hiyo katika utendaji wa kazi ni pamoja na kukosekana kwa ushahidi pindi kesi zinapokuwa mahakamani pamoja na ufinyu wa bajeti katika taasisi hiyo.“Moja ya changamoto ambazo zinaikabili taasisi hii ni pamoja na mashahidi kushindwa kufika kutoa ushahidi pindi kesi zinapokuwa mahakamani kesi nyingi zinafutwa kutokanna na kukosa ushahidi, pamoja na ufinyu wa bajeti katika kutekeleza majukumu yetu” amesema.