*********
NA EMMANUEL MBATILO
VETA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzania inafanikisha malengo ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hasa kutokana na kuhakikisha kila kukicha wanaibua teknolojia ambayo inaeleze uwepo wa viwanda hapa nchini.
Ameyasema hayo Mkurugenzi wa idara ya Elimu Mbdala na elimu ya Watu wazima Zanzibari Bi.Mashavu Fakh baada ya kutembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu NYerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Aidha Bi.Mashavu amewataka Wazanzibar waweze kuiga mfano kwa VETA hasa kwam mambo ambayo wanayafanya hasa kutekeleza malengo ya Serikali kufikia Uchumi wa Viwanda hasa tukitegemea viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa za hapa nchini.
Pamoja na hayo Bi.mashavu amesema kuwa hatua waliofikia VETA wanakwenda katika uchumi wa Viwanda kutokana na uzalishaji wa vijana wa kutumika sekta hiyo. Mashavu ameyasema vijana wanaopita VETA wanauwezo mkubwa katika sekta ya ajira kwa kujiajiri kutokana na ujuzi walioupata