Mmoja wa wanagenzi akimuelezea mteja ambaye ameweza kufika katika banda la VETA katika Maonesho ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya majiko ambayo yanatumia gesi yakiwa tayari kwa matumizi
*********
NA EMMANUEL MBATILO
Chuo cha Ufundi Stadi VETA wamebuni Teknolojia ya utumiaji wa jiko la gesi ambayo itasaidia kuondokana na uchafuzi wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti hobyo pamoja na kiafya kutokana na moshi pale unapotumia jiko la mkaa au kuni.
Ameyasema hayo leo mratibu wa mafunzo ya uwanagenzi VETA_Moshi, Bi.Theresia Ibrahimu baada ya Fullshangwe blog kutembelea banda la VETA katika viwanja vya Maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Haya majiko ya gesi yaliyobuniwa na Chuo Cha Ufundi VETA yataweza kuwarahisishia watumiaji kutumia bila kuchafua mazingira hasa katika suala la ukataji wa miti pamoja na kumkinga pale anapopika kwa kuwa jiko la gesi halitoi moshi hivyo hatuweza kudhulika kama atumiavyo majiko mengine”. Amesema Bi.Theresia.
Aidha Bi. Theresia ameongeza kuwa upatikanaji wa majiko hayo unaweza kuyapata kwa kupitia Chuo chochote cha Ufundi Stadi VETA na unaweza ukaletewa popote ulipo.
Hata hivyo Bi.Theresia amesema kuwa wamebuni pia blenda ya kusagia matunda na nafaka kwa urahisi ili kumrahishia mtumiaji asiweze kuhangaika kutumia blenda ambazo si salama na zisiszokuwa bora kwa matumizi.