Meneja Masoko wa Woiso Original Product Co Teya Herman akionesha viatu mbalimbali katika banda lao kwenye maonesho ya biashara ta Tantrade katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa Woiso Original Product Co Teya Herman akionesha ngozi zinazotumika kutengenezea viatu mbalimbali katika banda lao kwenye maonesho ya biashara ta Tantrade katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
……………………………………………..
MENEJA Masoko wa Woiso Original Product Co Teya Herman amesema wamefurahishwa kushika nafasi ya kwanza katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini huku akieleza namna ambavyo wamejinga katika kuunga mkono azma ya Serikali kuwa nchi ya viwanda kueleka uchumi wa kati.
Woiso ambao wamepiga kambi kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam wamekuwa wakivutia wananchi wengi kufika kwenye banda lao kutokana na ubora na ubunifu wa bidhaa zao zinazotokana na ngozi.
Akizungumza leo wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari , Teya Herman amesema bidhaa zote ambazo ziko kwenye maonesho ya Sabasaba zinatoka kwenye kampuni tanzu ya Himo Tanariz na kwamba ombi lao ni kuwataka Watanzania waitumie ngozi katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.
“Kupitia ngozi hiyo tunawahimiza wajasiriamali wadogo kutumia ngozi badala ya kutumia malighafi nyingine ambazo zinaisha haraka.Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwani ametupigania na kutuona kiasi cha kupata ushindi katika sekta ya ngozi kwa kuchukua kikombe cha mshindi wa kwanza,”amesema .
Pia amesema wanaishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na Mamlaka ya Biashara nchini (TANTRADE) kwa kuwaona na kutupatia zawadi ya kikombe.Wamewaomba waendelee hivyo hivyo kututia moyo.
Akizungumzia banda lao, amesema wanawakaribisha wananchi kutembelea banda la Woiso Original Product Co ili kupata bidhaa kwa bei nafuu kabisa.”Tunaomba Serikali iwatangazie Watanzania kuhusu umuhimu wa kuvaa bidhaa za ngozi kwani Watanzania wengi hawajui tofauti kati ya ngozi na bidhaa nyingine.”
Akifafanua zaidi kuhusu bidhaa zao amesema wao wako bega kwa began a Serikali na ndio maana wanapambana kupanua kiwanda chao na kuongeza uzalishaji kwa lengo la kutengeneza ajira zaidi kwa Watanzania.