Home Mchanganyiko TAASISI ya elimu ya Vyuo Vikuu vya Nje nchini Tanzania(UAR) yawakaribisha wanafunzi...

TAASISI ya elimu ya Vyuo Vikuu vya Nje nchini Tanzania(UAR) yawakaribisha wanafunzi wanaotaka kusoma vyuo vya nje

0

 

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya biashara ya Tantrade viwanja vya Mwalimu JK Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha akiwa pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo katika banda hilo.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la (UAR) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha  na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

……………………………………………………….

TAASISI inayowakilisha elimu ya Vyuo Vikuu vya Nje nchini Tanzania(UAR) imesema kwa sasa muitikio wa Watanzania kwenda kusoma nje ni mkubwa.

Pia ismesema wanafarajika kuwepo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es salaam kwani ni fursa kwao kutumia wingi wa watu wanaofika kwenye maonesho hayo kuzungumza nao.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha amesema hayo kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo nao wameweka banda kueleza shughuli wanazofanya.

 “Sisi kama taasisi tunathamini nakutambua mkusanyiko wa watu kwasababu kubwa mbili, kwanza sisi ni washauri kwa watanzania nini cha kusoma ukizingatia suala la ajira na tunatambua Vyuo vikuu vingi  vinafundisha elimu ya jumla(General Education).

“Kwa hiyo tumekuja na ufadhili wa masomo kutoka nje ya nchi lakini hatujakubali Scolashirp zote bali tumechagua zile ambazo zinaendana na mahitaji ya nchi kwa sasa kulingana na sera za nchi,”amesema Kabetha

Pia amesema wanatoa ushauri kwa Watanzania wakasome nini kuhusiana na hiyo sera ambayo itawapa ajira na itawatayarisha kwenye akili zao kwenda kujitegemea wao wenyewe.

“Kwa hiyo nafurahi kusema Serikali ya India na  Serikali ya China wametoa hizo Scola shirp zaidi ya 200  ambazo Watanzania watakwenda kusoma kwa gharama nafuu na ndogo sana na wengine watakwenda kusoma bure.

“Pia wengine watakwenda kusoma kwenye vyuo vikuu ambazo gharama zake ni sawa na vyuo vya Tanzania.Na masomo ambayo yamechaguliwa ni mambo ya teknolojia ya viwandani, mambo ya utengenezaji dawa , usindikaji na masomo yanayohusu biashara pamoja na aina nyingine ya masomo kulingana na mahitaji ya mhusika”amesema.

Ameongeza pia masomo ya teknolojia ya  kompyuta huku akifafanua hawajasahau masomo yanayohusu elimu ya tiba ya afya.Pia tumechukua wanafunzi wote wa masomo ya Art ili kwenda kusoma masomo mbalimbali,”amesema.

Hivyo amesema taasisi ya UAR inawakaribisha vijana wote waliomaliza ngazi ya  Diploma, Digrii na Mastars.Pia wale waliomaliza elimu ya kdato cha sita ambao wanajiandaa kwenda vyuo vikuu.

Akizungumzia muitikio wa Watanzania kwenda kusoma nje , amesema kwa sasa kwa sasa muitikio ni mkubwa kwani kila mmoja anataka kwenda kusoma nje na kuna maelfu ya Watu ya wanataka kwenda na changamoto inakuwa uwezo wa wazazi kwani wengine hawana hata nauli.

Hata hivyo amesema kutokana na muamko wa vijana wa Tanzania kwenda kusoma nje ya nchi kupitia taasisi yao kuna wazazi wamekuwa wakilipa kidogo kidogo na kufafanua changamoto iliyopo nafasi ni chache kuliko idadi ya wanaohitaji.

“Baada ya Maonesho ya Sabasaba tunapatikana pale Posta Mpya katika jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam.Ukifika kwenye jengo hilo nenda ghorofa ya kwanza na uliza UAR , basi utafikishwa tulipo. Pia tupo mikoani ambako nako tuna ofisi zetu,”amesema Kabetha.