Afisa Mahusiano Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Sarah Reuben akizungumza katika maonesho ya biashara ya Tantrade yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam leo.
………………………………………………..
NA EMMANUEL MBATILO
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umewaalika waajiri wote waliopo katika Tanzania Bara kujiunga na mfuko huo ili waweze kuondokana na hofu ya majanga yanayoweza kujitokeza mahala pa kazi.
Akizungumza katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bi. Sarah Reuben amesema kuwa wanasajili wanachama wapya na kutoa elimu ya kuhusu mafao pamoja na utaratibu wa kujiunga na mfuko huo.
“Tunao wataalamu wa kutosha kuweza kuwasajili wanachama wapya pamoja na kumuelimisha mtu kuhusu mafao yatolewayo na mfuko huu kwani hauitaji gharama yoyote hivyo wafanyakazi na wananchi wote tunawakaribisha”. Amesema Bi. Sarah.
Aidha Bi. Sarah amesema kuwa mfanyakazi atapata malipo hayo endapo atapata ugonjwa au majeraha yanayotokana na ajali kazini au ataugua kutokana na kazi na kumfanya apate ulemavu wa muda mfupi au wakudumu. Na iwapo mfanyakazi atafariki, fidia italipwa kwa wategemezi wake kwa mujibu wa Sheria.
Katika kufanya hivyo, moja kwa moja unampunguzia mzigo mwajiri wakushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi na kuwaondolea hofu wafanyakazi wanapokuwa wakitekelez majukumu yao.
Bi. Sarah Reuben amefafanua kuwa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi umeanzishwa ili kumsaidia mfanyakazi atakapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi anazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.
Mfuko huo uliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi (Sura 263 marejeo ya mwaka 2015).
Baadhi ya waajiriri wakiendelea kujisajiri katika mfuko huo kwa ajili ya wafanyakazi wao.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa tayari kupokea wananchi wanaotembelea katika banda hilo.
Banda linavyoonekana kwa ndani.
Ally Sheha ofisa wa usajili Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika banda la mfuko huo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya TANTRADE viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kirwa leo.