Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea katika banda la Chuo Kikuu cha Mzumbe kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Rainfrida Ngatuga
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
………………………………………………….
NA EMMANUEL MBATILO
Kutokuwepo na mfumo maalumu kwaajili ya kuwaleta madereva pamoja na wateja kusaidia kusafirisha mazao kutoka shambani kuleta viwandani hivyo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wameamua kuanzisha mfumo wa internet ambao unaitwa Trasms_Cargo ambao utamsaidia madereva kuwa[pata wateja wake sehemu yoyote ile.
Ameyasema hayo Mwanafunzi na Mjasiliamali kutoka katika Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro Bi. Angelina Emmanuel katika maonyesho ya biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maonyesho hayo Bi. Angelina amesema kuwa mfumo huo wa usafirishaji unasaidia kupunguza gharama kama vile mafuta kwa madereva pamoja na kumsaidia mteja kukusanya wateja wengine waweze kupakia mazao kwa pamoja kwa gharama nafuu.
“Mfumo huu utasaidia mazao mengi yaliyopo shambani kutokuweza kuharibika kwasababu ukiwa na akaunti ya Trasms-Cargo unaweza kupata usafiri ambao utasaidia kusafirisha mazao ya mkulima kwa haraka na nafuu”. Amesema Bi. Angelina.
Pamoja na hayo Bi. Angelina amesema kuwa apprication ya Transms-Cargo itakuwa inapatikana google internet pekee kwani mpaka sasa hawajaiweka katika google playstore.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Rainfrida Ngatuga amesema kuwa katika maonyesho hayo wao kama Chuo Kikuu Mzumbe wameamua kuleta bidhaa ambazo wametengeneza wanafunzi wa chuo hicho kwaajili ya kuonyesha baadhi ya jamii kufahamu.
“Tumekuja na wajasiliamali ambao wanaonyesha vitu vyao wanavitengeneza na wanaonyesha ni jinsi gani Chuo cha Mzumbe kinavyowasaidia kupanga biashara zao, kutekeleza na kuziuza kwa ustadi unaotakiwa”. Amesema Bi. Rainfrida.
Bidhaa ambazo tumeleta ni pamoja na asali ambazo zipo bora kwa matumizi na vilevile kuna bidhaa zingine ambazo wanafunzi wametengeneza kwaajili ya kuonyesha na kutambua ni namna gani wanafunzi wa chuo hicho wanaweza kufanya kitu kilivho bora kwa jamii kiujumla.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akizungumzana Mwanafunzi na Mjasiliamali kutoka katika Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro Bi. Angelina Emmanuel
Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Rainfrida Ngatugaakiwapa maelezo baadhi ya wananchi waliotembelea banda la chuo hicho leo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Bw. Godfred Mbanyi akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi hao.
Rose Joseph Afisa mawasiliano Mwandamizi Chuo Kikuu cha Muzumbe akiwa katika banda hilo kwa ajili ya kuhudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea katika maonesho hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiwa tayari kwa kutoa maelezo mbalimbali kuhusu shughuli zinazofanywa na chuo hicho.