Badru Idd Meneja wa kanda ya Kaskazini Benki ya NMB akizugumza na waandishi wa Habari kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda Hilo katika maonesho ya biashara ya ya Kimataifa Tantrade viwanja vya Mawlimu Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam, kushoto ni Kidawa Masoud Meneja wa tawi la NMB katika maonyesho hayo.
Badru Idd Meneja wa kanda ya Kaskazini Benki ya NMBamesema benki hiyo inatoa huduma za aina mbalimbali katika maonesho hayo ili kuwapa fursa mbalimbali wateja watakaohitaji huduma ya kifedha katika maonesho hayo
Ameongeza kuwa hata ukihitaji fedha mbalimbali za kigeni kwa kiwango unachohitaji jambo kubwa ni kwenda kuwaona katika tawi lao la Sabasaba na wao watakubadilishia fedha zako ili uendelee na shughuli zako.
Amesema tunajua kuna wageni kutoka mataifa mbalimbali ambao wanahudhuria katika maonesho hayo hivyo wasipate shida kubwa ni kwenda katika yawil la NMB Sabasaba na watapata huduma ya kubadilisha fedha zao ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti.
Kidawa Masoud Meneja wa tawi la NMB katika Banda la Benki hiyo kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya Tantrade viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam akizugumza na waandishi wa Habari kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda Hilo , Kutoka kulia ni Vicent Mnyanyika Meneja wa mawasiliano NMB na Badru Idd Meneja wa kanda ya Kazkazini NMB.