*************
Ofisi ya waziri mkuu inayoshughulikia sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana wenye Ulemavu imefanya ziara katika mikoa mbalimbali pamoja na Halmashauri nchini ili kufanya tathmini ya utekelezaji wa Programu za kimaendeleo za vijana, changamoto pamoja na kubaini fursa zilizopo katika mikoa na wilaya.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hiili Kaimu mkurugenzi Ukuzaji Bibi Venerose Mtenga amesema program hii iliyozinduliwa tarehe 11 inaendelea na zoezi la kubaini changamoto za vijana katika mikoa na halmashauri zote nchini iili kuweza kuandaa mkakati wa pamoja na namna ya kutatua changamoto hizo pamoja na kuandaa mkakati mzuri wa namna ya kuratibu shughuli za kuwezesha vijana kiuchumi.
Bibi Venerose amesema katika zoezi hilo pamoja na mambo mengine wataalamu hao watatembelea na kukagua miradi ya uzalishaji mali ya vikundi vya vijana pamoja na kutathmini hali halisi ya utekelezaji program za kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu
Aidha thathimiini hii pia inalenga kufuatilia marejessho ya fedha zilizokopeshwa kwa vijana kupitia mfuko wa Maendeleo ya Vijana, kubaini fursa za ajira ziilizopo katika Halmashauri, wadau mbalimbali wanaoshiriki katika program zakuwawezesha vijana na kupendekeza namna nzuri ya kuboresha mahusiano na ushirikiano na wadau hao.
Ameongeza pia miradi mingine inayotembelewa ni pamoja na Kilimo cha umwagiliaji kwa teknolojia ya kitalu nyumba unaotekelezwa na Halmashaurii zote nchini, ametaja miradi mingine ni Mabwawa ya samaki, Ushonaji, ufugaji nyuki pamoja na uchomeleaj vyuma
Akizungumzia upande wa changamoto kaimu mkurugenzi huyo amesema marejesho ya mikopo kwa upande wa vijana ni changamoto kubwa, baadhi ya vijana wamekuwa wakihama makazi yao na kwenda sehemu nyiingine mara tu baada ya kupokea mikopo na hivyo kufanya suala la marejesho kuwa gumu na baadhi ya viikundi kusambaratika, anasema uaminifu kwa vijana ni mdogo ukilinganisha na kina wanawake
Pia mabadiliko ya hali ya hewa mwaka huu yameongeza changamoto kuwa kubwa hasa kwa vikundi vya kilimo, vijana wameeleza sababu ya kutotekeleza miradi kwa ufanisi wakatii mwingine kunasababishwa na ucheleweshaji wa fedha katika, vilevile fedha inayotoka kwa ajili ya mikopo ni kidogo, haikidhi mahitaji na kusababisha kutofikiwa kwa malengo ya miradi iliyokusudiwa na vikundi, suala liingiine lililojitokeza ni kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali pamoja na uwepo wa masoko ya biidhaa imekuwa changamoto kubwa inayosababisha kudororakwa vikundi viingi.
Mafanikio kwa vikundi vilivyokopeshwa baada ya kutembelewa katika baadhi ya mikoa kama vile Dodoma na singida ni pamoja na kukuza mitaji na kujenga uwezo wa kibiashara, kuaminika na kupewa zabuni mbalimbali hasa kwa vikundi vya ufundi.
Kwa upande wa vikundii ya kina wanawake wamefanikiwa kulipa ada za watoto
mashuleni na kuboresha lishe na ustawi wa familia kwa ujumla na hiyo kujenga tabia ya kujiamini zaidi na kuondoa utegemezi kwa waume zao