Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ameweka bayana kuanza kwa Ujenzi wa Barabara ya Tanga, Pangani, Saadan, Bagamoyo.
Mh.Kamwelwe amekiri kuwa mfupa ulioshindwa kutafunika muda mrefu umepata fisi sahihi baada ya Mhe. Rais Dk.John Pombe Magufuli kutoa fedha kuidhinisha ujenzi wa barabara hiyo.
Aidha Mhe. Waziri ameweka wazi kuwa kiuhalisia maandalizi yote ya awali yamefanyika, tathimini na uhakiki wa fidia upo mwishoni, fedha zimeshaingia na mkandarasi ameshapatikana zaidi kufikia mwezi huu wa sita mkataba utakua umesainiwa na hatua za ujenzi zitaanza.