Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI WA NISHATI AWASHA UMEME KATIKA KIJIJI CHA CHIBWEGERE WILAYANI MPWAPWA...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AWASHA UMEME KATIKA KIJIJI CHA CHIBWEGERE WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA

0

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Chibwegere kwa ajili ya kuwasha umeme upande wa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri.

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chibwegere wakati wa hafla ya kuwasha umeme ambapo Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu amekata utepe wa kuwasha umeme.

Meneja wa Wilaya ya Mpwapwa Beatus Kabwe,akisoma taarifa kwa mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara ya kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere.

Mbunge wa jimbo la Kibakwe George Simbachawene,akizungumza na wanachi wa kijiji cha Chibwegere kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu ambaye alifanya ziara ya kuwasha umeme katika kijiji hicho

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chibwegere alipokuwa amefanya ziara ya kuwasha umeme kulia kwake ni Mbunge wa jimbo la Kibakwe George Simbachawene na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri.

Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Chibwegere wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu (hayupo pichani) leo alipofanya ziara ya kuwasha umeme katika kijiji hicho.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma leo Mei 24,2019.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na wananchi wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Mei 24,2019.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu,akiwaonesha wananchi kifaa cha umeme (UMETA) wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma leo Mei 24,2019.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu,akikata utepe kwa ajili ya uzinduzi wa kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Mei 24,2019.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akiwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma alipofanya ziara leo Mei 24,2019.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

……………………

Na.Alex Sonna,Mpwapwa

Ikumbukwe kuwa Mei 7,2019 WAZIRI wa Nishati, Dk.Medard Kaleman aliagiza kukamatwa na kutiwa mbaloni kwa Mkandarasi wa kampuni ya OK Electrical Contractor  aliyekuwa akisambaza umeme wa mradi wa REA awamu ya III katika wilaya ya Mpwapwa kutokana na kutokamilisha kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere

Hatimaye leo Mei 24,2019 Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu  amefanya ziara ya kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ikiwa ni juhudi za Serikali za kuhakikisha kila mwananchi aweze kuunganishiwa umeme.

Mhe.Mgalu akizungumza na wananchi huku akitoa elimu kuhusu gharama za kuwaunganishia umeme amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli inawajibu ya kuwajali na kuwathamini wananchi wa kipato cha chini.

Amesema kuwa Serikali imeamua kushusha gharama za kuwaunganishia umeme wananchi wake hadi shilingi 27,000/= tu.

“Hapo mwanzo gharama za kuunganishiwa umeme zilikuwa ni shilingi 177,000, lakini Serikali kwa vile inawajali wananchi wake imelipa shilingi 150,000/= kwa kila anayeweka umeme, na kazi ya mwananchi ni kulipia kiasi kidogo tu cha shilingi 27,000/=, tofauti na hapo awali.” amesema Mhe.Mgalu

Aidha amesema kuwa wapo wananchi wanaoishi karibu na miundombinu ya njia ya umeme na sio kwamba wanashindwa kulipa shilingi elfu 27,000/= bali wanashindwa na gharama ya kutandaza umeme ndani ya nyumba (wiring) inayofanywa na wakandarasi.(mafundi).

“Gharama hizo za wiring zimeonekana kuwa ndio changamoto kwa wananchi na serikali imepokea changamoto hizo na kuwa itazifanyia kazi.” amesisitiza

Naibu Waziri huyo ameutaka  uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Dodoma na Mpwapwa kuhakikisha wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa wanakijiji ili waweze kunufaika na huduma hiyo.

Aidha Mhe.Mgalu amefafanua kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafikisha huduma ya umeme kwa wananchi ambapo hadi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wamekamilisha kazi hiyo ya kusambaza umeme vijijini nchi nzima na kubakiza kazi ya kuwaunganishia wananchi

Naye Mbunge wa jimbo la Kibakwe George Simbachawene, ameishukuru serikali kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwasambazia wananchi umeme na kusema kuwa maendeleo yanakua kwa kasi kubwa inayotokana na kasi ya Rais, Dk.John Magufuli ya kuwajali wananchi hasa wenye hali ya chini.

Alimuomba Naibu waziri kuwapelekea umeme wananchi wa kijiji cha Msisili ambacho kipo jirani na Chibwegele ili nao waweze kupata huduma hiyo.

Jimbo la Kibakwe mpaka sasa vijiji 42 tayari vimeshapata umeme huku vikibaki vijiji vinane ambavyo bado havijapata umeme huku Serikali ikiendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa hadi Disemba vitakuwa tayari vimeshapata umeme