Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) leo, Novemba 24, 2026. imerejesha ushindi na ubingwa wa AFCON 2025 kwa Senegal leo
Uamuzi huo umetolewa baada ya CAS kutengua uamuzi wa awali wa Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) uliokuwa umeivua Senegal ubingwa na kuipa Morocco ushindi wa mezani.
Uamuzi huu umeongozwa na Jopo la majaji watatu wa CAS jijini Lausanne umelikubali shauri la rufaa la Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) na kuthibitisha kuwa Senegal ndio mabingwa wa Afrika.
Katika fainali iliyochezwa mjini Rabat, Senegal ilishinda bao 1-0 dhidi ya Morocco kupitia bao la muda wa nyongeza la Pape Gueye.
Hata hivyo, wachezaji wa Senegal walikuwa wameondoka uwanjani kwa takribani dakika 14 kupinga penalti iliyotolewa kwa Morocco (ambayo Brahim Diaz alikosa) kabla ya kurejea kuendelea na mchezo.
Uamuzi wa CAF (Machi 2026): Miezi miwili baada ya fainali, CAF ilitangaza kuwa Senegal ilipoteza mchezo kwa kukiuka kanuni za kuondoka uwanjani, na kuipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0.
