Pambano la Ngumi za kulipwa na Ridhaa litakaloshirikisha Mabondia mbalimbali nchini wakiwemo wa Jeshi la Kujenga Taifa na Ngome linatarajia kupigwa Juni 7 Mwaka huu katika Ukumbi wa Club 361 Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mratibu wa Ufundi wa pambano hilo Yassin Abdalah Ustaadh alisema upinzani wa JKT na Ngome ni wa kihistoria hivyo watu waje waaangalie burudani Nzuri ya Ngumi.
“ Mabondi wazuri wa Ngumi za kulipwa ni wale walioanzia Ngumi za Ridhaa na Kuwepo kwa JKT na Ngome katika Pambano hilo ni hatua muhimu na Mchango Mkubwa wa jeshi katika Kuendelelea Ngumi na michezo kwa Ujumla.” Alisema Ustaadh.
Aliwataka mabondia wa Ngumi za kulipwa kuwa ni Nassib Ramadhani atakayezichapa na Mohamed Kashinde wakati Kiasi Ally ananyukana na Shadrack Ignas wakati Kudura Tamimu atazichapa na Baina Mazola.
Aliongeza kuwa pambano lingine ni la kuvutia lenye lengo la kuvunja Historia ya Japhet Kaseba kumkaribisha katika Ngumi Mchezaji wa Ngumi na mateke Jeremia Jackson atakayecheza na Hashim Masungo.
Kwa upande wa Kocha wa Ngome Mteule daraja la pili Hassan mzonge alisema wamejiandaa vyema na Mmoja wa mabondi watakopambana katika uzito wa Kilo 81 ni Koplo Selemani Kidunda na kutuma salamu kwa JKT.
Kwa Upande wake katibu wa kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Yahaya Poli alipongeza waaandaji kutekeleza sera ya kamisheni kuchanganya mapambano ya kulipwa na Ridhaa na Kibali kimetolewa kwa ajili ya kufanyika kwa Pambano hilo.
Kwa Upande wa Wadhamini wa pambano hilo kampuni ya Euromax kupitia kwa Afisa masoko wake Forgiver Tito aliahidi wapenzi wa Ngumi kuwa kuwa Wataendelea kusaidia kukuza mchezo huo kwani ni sehemu ya Ajira na kuwataka wadhamini wengine kujitokeza.
Naye Mratibu wa Pambano hilo Beatrice Ntahona alisema Maandalizi yote yamekamilika na watakahikisha unapatikana ulingo mzuri na mandhari yatakuwa mazuri kuhakikisha mabondia wanacheza vizuri na kupata mshindi halali.
Mapambano hayo ya Ngumi yasiyo ya Ubingwa yanalengo la kuendeleza vipaji vya ngumi za kulipwa nchini sambamba na kuwa sehemu ya Matayarisho kwa Vilabu vya ngumi za Jeshi zinazojiandaa na Mashindano mbalimbali ndani na Nje ya Nchi.