Home Mchanganyiko Basi la Arusha Express lateketea kwa moto

Basi la Arusha Express lateketea kwa moto

0

Basi  la Arusha Express ambalo linafanya safari zake kati ya Bukoba na Arusha limeteketea kwa moto kwenye eneo la Kibeta katika  Manispaa ya Bukoba  muda mfupi tu baada ya kuanza safari yake kuelekea Arusha.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema hakuna mtu aliejeruhiwa wala kupoteza maisha isipouwa watu wamepoteza mali zao ambazo zimeteketea kwa mto ndani ya basi hilo.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanaendelea kusema Abiria alipatwa na kiwewe baada ya Basi hilo kushika moto na kuanza kuungua huku wakijaribu kujiokoa kutoka ndani ya basi hilo 

Hata hivy abiria wote waliokolewa kasoro mizigo yao na vitu mbalimbali vilivyoteketea kabisa pamoja na basi hilo.